Serikali
kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi inatarajia
kujenga Vyuo vya Ufundi (VETA) kwa kila wilaya ili kutoa fursa kwa
wananchi wengi hususani vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ufundi
yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa.
Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya wakati akijibu
swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu
ujenzi wa vyuo vya VETA kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja
kati ya Wilaya kumi za mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo
hivyo .
Naibu Waziri huyo amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo hicho Cha VETA , tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika yamekamilika.
Naibu Waziri huyo amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo hicho Cha VETA , tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika yamekamilika.
“Natoa
wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na Halmashauri za
Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi
wa vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute eneo lipo
tayari kwa kuanza utekelezaji wake”Alisema Mhe.Manyanya.
Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 Wizara hiyo
kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshateua wataalamu
elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la jinsi ya kuifanya kazi
ya kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo ili kuanza ujenzi mara
moja.
Serikali
kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa kushirikiana
na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga kutoa elimu bora
ya ufundi yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya ufundi stadi nchini
ili kuwawezesha wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa maendeleo yao na
taifa kwa ujumla.
Post a Comment