Featured

Loading...


TRENI YA MWAKYEMBE DAR YASITISHWA GHAFLA, WANANCHI WALALAMIKA

JIJI la Dar es Salaam ambalo lilikuwa limepiga hatua ya maendeleo kwa kuwa na treni ya mjini, limepata pigo baada ya huduma ya usafiri wa treni hiyo kusitishwa.
Wiki iliyopita nilipata nafasi na kwenda kuchunguza kama kweli treni hiyo ya kutoka Ubungo hadi katikati ya mji kama kweli huduma imesitishwa, nikathibitishiwa kuwa kweli hakuna usafiri huo.
Kama Mwanafukunyua Fukunyua, nilijitahidi kuwahoji askari waliokuwepo kwenye Stesheni ya Ubungo ili kujua kulikoni usafiri wetu walalahoi haupo.
Askari yule niliyemhoji ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini alinijibu kwamba kwa muda mrefu sasa usafiri huo wa kutoka Ubungo hadi Stesheni, umesitishwa.
“Umesitishwa? Mbona hatujatangaziwa?” nilimhoji. Alijibu kwamba yeye hajui lolote.
Nilijaribu kuwahoji wananchi wenzangu waliokuwepo eneo hilo kama ni kweli niliyoambiwa na askari yule au alikuwa akinitania.
Mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Somoe Hamisi, alisema ni kweli kwa siku kadhaa treni hiyo haifiki Ubungo na kusababisha adha kubwa kwa wananchi wa kawaida.“Sisi watu wazima imetuathiri lakini walioathirika zaidi ni watoto wa shule kwa sababu hii treni ilikuwa inawachukua bila kusukumwa kama wanavyofanyiwa kwenye daladala.
“Nchi hii inashangaza, waziri fulani akifanya kazi nzuri kwenye sekta fulani, wanamuonea wivu na baada ya siku chache anahamishwa. Ndivyo alivyofanyiwa Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alitukomboa, sasa treni tunaambiwa haipo,” alilalamika Somoe.
Naye Aloyce Shirima ambaye alisema ni mfanyabiashara anasema treni hiyo ilikuwa ikimsaidia sana.
“Nilikuwa nikinunua bidhaa zangu Kisutu, nakwenda kupanda treni hadi Ubungo, kisha kuja Mwenge kwenye biashara zangu. Tangu isitishwe ni shida kubwa sana,” alisema Shirima.
Hamisi Ali alisema treni hiyo ilikuwa ikiwasaidia sana kwani sasa wanapoteza muda mwingi kwenye madaladala hivyo kuathirika kiuchumi.Safu hii ilimtuma mwandishi wake hadi kwa Msemaji wa Shirika la Reli (TRL), Midlady Maez ambaye alikiri kuwa huduma hiyo imesitishwa.
“Bado ukarabati unaendelea, hivyo huduma hiyo itaanza kazi itakapomalizika. Injini zote mbili zipo kwenye karakana kubwa ya Morogoro.“Mafundi wanaendelea na marekebisho, zitakapokuwa tayari usafiri utarejea kama kawaida,” alisema msemaji huyo wa TRL.
Alipoulizwa ni lini usafiri huo utakuwa tayari au ukarabati utamalizika, Maez alisema hawezi kutolea ufafanuzi suala hilo kwa kuwa mafundi bado wanaendelea na kazi. Aliwataka wananchi kuwa na uvumilivu.
Wakati TRL ikisitisha huduma hiyo ya treni kwa muda, Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) wao huduma yao ya treni kutoka Stesheni ya Tazara hadi  Mwakanga, Kigogo Fresh, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, inaendelea.Kuna treni ya kutoka Tazara ya saa 10 jioni, saa 12 jioni na ingine hutoka katika kituo hicho saa mbili usiku.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top