Jeshi
la Polisi nchini linafanya uchunguzi kumbaini mmiliki wa ukurasa wa
twitter unaoendeshwa na anayejiita Daudi Balali, aliyewahi kuwa Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi
yake.
Mkurugenzi
wa Habari na Mahusiano wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba, aliyasema
hayo wakati akizungumza na Gazeti la Nipashe ofisini kwake jana.
Bulimba
alisema kuwa taarifa za uwapo wa ukurasa huo wa twitter,
wamekwishazipata na wanafanya uchunguzi wa kina kumkamata mhusika kisha
kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
“Tunazo
taarifa juu ya ukurasa huo wenye wafuasi wengi kwa sasa na unaotumika
kuwashambulia viongozi wa serikali na wa siasa hasa wale wanaogombea
nafasi kubwa za utawala nchini, hivyo Jeshi la Polisi lipo kwenye
uchunguzi ili kumbaini mtu huyo haraka iwezekanavyo,” alisisitiza Senso.
Ukurasa
huo ulioanza kutumika kabla ya Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni kuanza
kutumika, una wafuasi zaidi ya 6,000 kwa sasa na umekuwa ukitumika
kuwachafua wagombea urais nchini hasa wa upinzani.
Aidha, umekuwa ukitabiri matokeo ya uchaguzi, kitendo ambacho kimekuwa kikiwachanganya wananchi.
Bulimba alisisitiza kuwa jeshi hilo liko makini na linafuatilia hivyo mtu huyo atasakwa na kukamatwa akiwa mahali popote.
Aliwataka
pia wananchi kuripoti katika vituo vya polisi pindi wanapopata vitisho
vya aina yoyote, kudhalilishwa ama kufanyiwa kitu chochote kibaya
kupitia mitandao ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
“Jeshi
la polisi linafanya kazi usiku na mchana, hivyo mtu yeyote
asijidanganye kwamba atavunja sheria na asikamatwe, maana tuna njia
nyingi za kuwabaini watu hao kwa kushirikiana vyema na TCRA pamoja na
wananchi, hivyo chanzo chochote kinachohusu uhalifu wa mtandaoni,
kitashughulikiwa,” aliongeza.
Aliwaonya
pia watu waliokuwa wakitumia kurasa mbalimbali kwenye mitandao ya
kijamii kwa kutumia majina ya watu wengine ili kudhalilisha watu na
kupotosha umma kwa kutoa taarifa za uongo juu ya masuala mbalimbali
kuachana mara moja na tabia hiyo maana wakibainika watachukuliwa hatua
kali za kisheria na kuwa mfano kwa wengine wanaojihusisha na vitendo
hivyo.
~Mpekuzi blog
Post a Comment