Umoja
wa katiba ya wananchi Tanzania UKAWA umeitaka taasisi inayijihusisha
na maswala ya midahalo na tafiti mbalimbali TWAWEZA kuandaa mdahalo wa
wazi na umoja huo kwa ajili ya kuichambua na kuitetea tafiti yao
waliyoitoa hivi majuzi inayoonyesha kuwa chama cha mapinduzi kina nafasi
kubwa ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Akizungumza
na wanahabari jana kuhusu kile alichokiita kuwa ni utafiti wa kupikwa
kwa maslahi ya watu,mwenyekiti mwenza wa umoja huo JAMES MBATIA alisema
kuwa TWAWEZA kama Taasisi inayojihusisha na uandaaji wa midahalo na
kufadhili midahalo mbalimbali inayohusiana na uchaguzi mkuu wanawataka
kuitisha mdahalo baina yao na viongozi wa umoja huo kwa ajili ya
kuitetea taarifa yao hiyo.
Akizngumzia
Taarifa hiyo ya TWAWEZA mh MBATIA alisema kuwa ni jambo jema kwa
taasisi hiyo kushiriki katika maswala ya kukuza Demokrasia ya Tanzania
lakini wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa iliyotolewa na taaisis
hiyo kutokana na kuonekana ina mapungufu mengi ya wazi ambayo hata mtu
ambaye hajasoma anaona wazi kuwa ni utafiti wa kupikwa kwa ajili ya
maslahi ya chama cha mapinduzi.
Mbatia alisema taarifa hiyo inaonyesha wazi jinsi gani taasisi hiyo inatumika vibaya na chama cha mapinduzi kwa ajili ya kuwaahadaa wapiga kura na kawaaminisha kuwa chama cha mapinduzi bado kina uwezo wa kushinda.
Mbatia alisema taarifa hiyo inaonyesha wazi jinsi gani taasisi hiyo inatumika vibaya na chama cha mapinduzi kwa ajili ya kuwaahadaa wapiga kura na kawaaminisha kuwa chama cha mapinduzi bado kina uwezo wa kushinda.
Alisema
kuwa pamoja na Taarifa zote lakini ni wazi kuwa taarifa hiyo imejaa
propaganda ambazo moja kwa moja zimelenga kukisaidia chama cha mapinduzi
ambapo amesema kuwa jambo hilo limeidhalilisha sana taasisi hiyo.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa kuna kasoro nyingi ambazo zipo katika utafiti huo na
kufanya watanzania kupuuza utafiti huo huku akizitaja kadhaa kuwa ni –
1-Waliotafitiwa
walipewa simu za bure na watoa utafiti,ambapo katika taarifa hiyo
imeandikwa kuwa simu za mkononi pamoja na chaja,zinazotumia chaji mwanga
wa jua ziligawiwa kwa kaya shiriki.
2-Watafiti
wenyewe wanaonekana kudhani kuwa UKAWA ni chama ambapo katika ukarasa
wa kwanza wa taarifa hiyo mgombea anayewakilisha ukawa ni EDWARD LOWASA.
3-Kutothamini
kwa usawa,michango,ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi huu mkuu,vyama kama
ADC,CHAUMA,NLD,NRA,na UPDP havikuwekewa takwimu za moja kwa moja ambapo
vilihesabika kama vyama vingine.
4-Kuorodhesha vyama visivyokuwa na wagombea Urais katika swali la kuchagua Rais kwa mfano CUF,NCCR-MAGEUZI.
5-Maana ya UKAWA ni “Walinzi wa katiba ya wananchi” ndivyo utafiti unavyoeleza katika uk 11 aya ya kwanza.
6-Jumla
ya asilimia kwa wima kutokuwa 100,katika kila jedwali kwenye ukurasa wa
8,9 na 10 kwa mfano kwenye jedwali ukurasa wa 8,jumla nya asilimia
chini ya mwaka 2013 ni 82badala ya 100,kwenye jedwali la ukurasa
9,ujumla chini ya mwaka 2015 ni 102,kwenye jedwali la ukurasa wa 10
jumla chini ya mwaka 2014 ni 85
7-Mtafiti
hawezi kutafiti kitu anachokijua ambapo katika ukurasa wa 10 imeandikwa
ikumbukwe kuwa UKAWA imejumuishwa katika kielelezo hiki ili kuonyesha
kuwa wananchi wanadhani kwamba UKAWA ni chama ,UKAWA haijasajiliwa kama
chama cha siasa
8-Majumuisho
ya Matokeo ya utafiti hayaendani na maswali ya utafiti kwa mfano katika
ukurasa wa 7 swali ni Je uchaguzi ungefanyika leo ungempigia kura
mgombea wa chama gani,wakati jumuisho la tafiti huo linasema kuwa CCM
ndio chama kinachopendwa zaidi na wanaowaunga mkono CHADEMA wamepungua
kidogo tangu mwaka 2013.
9-Kauli nyingi zinakinzana mfano;
(A)
Katika ukurasa wa 12 imeandikwa kuwa utafitri huu sio utabiri lakini
katika majumuisho katika ukurasa wa 15 imeandikwa kuwa “karibu wananchi
wote 99% wanasema kuwa watapiga kura katika”
“Zaidi ya 60% walisema kuwa watamchagua mgombea wa CCM wa Urais,ubunge na udiwani”
“26% ya wananchi watamchagua kwa sababu hii..
B) Katika Ukurasa wa 12 swali lilikuwa “ukimwacha Rais Kikwete iwapo uchaguzi wa rais ungefanyika leo ungemchagua nani?”
“Chanzo cha takwimu wahojiwa hawakupatiwa orodha ya kuchagua
Mh
MBATIA alisema kuwa kutokana na maswala hayo yaliyojitokeza ni wazi
kuwa utafiti huo hauna nia njema kwa uchaguzi wa mwaka huu,huku
akiwaomba watanzania pamoja na wapenda maendeleo na mabadiliko
kutoitilia maanani Taarifa hiyo na kuwataka watanzania waendelee
kuilinda na kuitunza amani kwani tafiti kama hizo za kupikwa zinaweza
kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani kwa watanzania.
Hapo chini kuna video:
Hapo chini kuna video:

Post a Comment