Featured

Loading...


Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo Aahidi Kumteua Magufuli Kuwa Waziri wa Ujenzi


Mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, Anna Mghwira amesema akipata ridhaa ya wananchi kuwa rais wa Tanzania, atamteua mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kuwa Waziri wa Ujenzi.

Akizungumza kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni zake kwa Mkoa wa Arusha, mgombea huyo alisema Dk Magufuli ni mtendaji ndiyo maana anasisitiza kujenga madaraja na barabara kila anakokwenda.

“Kazi ya rais si kujenga barabara, sasa kwa kuwa yeye yuko vizuri katika suala la ujenzi nichagueni niwe rais wenu ili nije kumchagua aendelee kujenga barabara, kazi anayoifanya kwa ufanisi,” alisisitiza.

Awali, katika mikutano aliyofanya katika majimbo ya Arumeru Magharibi, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini, mgombea huyo alisema Serikali yake ina sera mahsusi kwa ajili ya wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye utajiri mkubwa nchini ukiwa umezungukwa na rasilimali mbalimbali.

Alisema mkoa huo pekee wenye madini ya Tanzanite nchini na duniani kwa ujumla, pia una mbuga mbalimbali za wanyama.

Kwa upande wa kilimo, alisema mazao kama kahawa, maua, vitunguu maji na mbogamboga ni vipaumbele vyake.

“Tunataka Watanzania wajiwekee akiba ili tutunishe mifuko ya hifadhi ya jamii. Katika utawala wetu tunataka watu milioni tano waingie kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kipindi cha mwezi mmoja,” alisema na kuongeza:

“Ukiweka Sh10,000 Serikali itakuongezea Sh20,000, hivyo kila mwezi utakuwa na uhakika wa kuingiza Sh30,000,” alisema.

Alisema mfumo wa maisha ya Watanzania unahitaji kufanyiwa mabadiliko na wao ndio wanaopaswa kusimamia suala hilo.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top