
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha
Mbede Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi amekamatwa akiwa na meno ya Tembo
nane yenye uzito wa kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni
120 ambapo ni sawa na Tembo wanne waliuwawa.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa
Habari kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mida ya saa tatu na nusu .
Kidavashari
alisema mtuhumiwa Ndizu alikamatwa kufuatia misako na uparesheni
mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi ikiwa ni
kuhakikisha wahalifu wa makosa mbalimbali wakimemo wawindaji haramu wa
wanyama pori wanakamatwa.
Siku
hiyo ya tukio jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa Raia wema kuwa
katika pori la akiba la Lwafe kuna watu wanajihusisha na biashara haramu
ya meno ya Tembo .
Kidavashari
aliendelea kuwaambia waandishi wa Habari baada ya taarifa hizo
kupokelewa ufuatiliaji ulifanyika kwa polisi kufika kwenye eneo hilo na
kuweka mtego ambapo walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Nzuri Ndizu
akiwa na meno ya Tembo vipande nane akiwa ameyaficha kwenye pori kwa
ajili ya kusubiria wateja .
Kamanda
Kidavashari alisema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi
kwa hatua za upelelezi zaidi ilikuendelea kubaini mitandao yote
inayojihusisha na biashara hiyo haramu ya meno ya Tembo na kufikishwa
Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika .
Post a Comment