Featured

Loading...


Msimamizi Wa BomoaBomoa Dar Aanguka Ghafla Ofisini Kwake.... Madaktari Washindwa Kubaini Tatizo


Operesheni kubwa ya kubomoa nyumba zaidi ya 15,000 zilizojengwa katika maeneo yasiyostahili jijini Dar es Salaam, imekumbana na changamoto ya aina yake baada ya mmoja wa wasimamizi wa kazi hiyo kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (Nemc), Heche Suguti, kuanguka ghafla akiwa ofisini kwake na kuwahishwa hospitali akiwa hoi.

Chanzo  kutoka ndani ya Nemc kimesema kuwa Suguti ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika baraza hilo, alianguka ofisini kwake majira ya saa 9:30 alasiri baada ya kurejea kutoka katika Mahakama Kuu kitengo cha ardhi kushughulikia kesi inayoikabili Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi dhidi ya wakazi 681 wa eneo la Mkwajuni, Kinondoni ambao wanapinga nyumba zao kubomolewa.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya Suguti kuanguka ghafla ofisini kwake eneo la Mikocheni, baadhi ya wafanyakazi wenzake (wa Nemc) walimsaidia haraka kwa kumbeba na kumpakiza kwenye gari na kumpeleka hospitali mbili tofauti ambako kote vipimo vya awali havikubaini tatizo.

“Baadaye alipelekwa katika Hospitali ya Aga Khan ambako alilazwa kuanzia siku hiyo (Jumanne) na kutolewa leo asubuhi (jana) baada ya kupata nafuu… ila kwa kifupi ni kwamba afya yake imeyumba na hadi sasa madaktari bado wanachunguza kujua ni kitu gani hasa kinachomsumbua,” chanzo kiliiambia Nipashe jana.

Mkurugenzi wa Nemc, Bonaventure Baya, alikiri kuwa Suguti aliugua baada ya kuanguka ofisini Jumanne wiki hii na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan, lakini haoni kama ni sahihi kuzungumzia afya yake kwani hayo ni masuala binafsi.

 “Nadhani ni uchovu ndiyo uliokuwa unamsumbua… hata hivyo, hayo ni masuala binafsi.  "

Alipotafutwa kwa njia ya simu jana mchana, Suguti aliyekuwa akizungumza kwa taabu, alikiri kupatwa na tatizo asilolifahamu na kuanguka ofisini kabla ya kujikuta akiwa amelazwa katika wodi mojawapo ya Hospitali ya Aga Khan.

“Kwakweli sielewi kilichotokea. Nilipoingia ofisini kwangu baada ya kutoka kwenye kesi ya nyumba za watu wa Kinondoni, ghafla nikahisi kizunguzungu, giza kutanda na mwishowe nikaanguka… sijui kilichotokea baada ya hapo ila fahamu ziliponirudia nikajikuta nikiwa hospitali,” alisema Suguti.
 
Alipotakiwa kueleza zaidi kuhusiana na tukio hilo, Suguti hakuwa tayari kwa maelezo kuwa bado hajisikii vizuri.

“Kwa sasa naomba uniache tu, sijisikii kuzungumza zaidi,” alisema na kukata simu.

Zaidi ya nyumba 16,000 zimeshawekwa alama ya X katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambazo zinatakiwa kubomolewa kutokana na kujengwa maeneo hatarishi.

Credit: Nipashe

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top