Featured

Loading...


Rais Magufuli Amng'oa Eliakim Maswi TRA Na Kumrudisha Manyara ....Awafuta Kazi Vigogo Wawili Idara Ya Uhamiaji


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Bwana Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bwana Piniel Mgonja   ili kupisha uchunguzi, kufuatia dosari alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amezitaja dosari hizo kuwa ni pamoja na tuhuma za rushwa, ukusanyaji mbaya wa maduhuli ya serikali, ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na utendaji mbovu.

Balozi Sefue amesema watendaji hao wakuu wa Uhamiaji wamesimamishwa kazi mara moja hadi hapo uchunguzi utakapokamilika na kwamba endapo watabainika kutokuwa na makosa Rais ataamua hatma yao.

Katika Hatua nyingine Rais John Pombe Magufuli amemrejesha Bwana Eliakim Chacha Maswi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, baada ya kukamilisha kazi maalum aliyomtuma kuifanya katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kabla ya kurejeshwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana Maswi aliteuliwa kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo kwa lengo la kumtafuta mtu mwenye utaalamu wa kuendeleza kazi iliyofanywa na Bwana Maswi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
20 Januari, 2016  

==>Msikilize Katibu Mkuu  Kiongozi Akiongea

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top