
Serikali
imesema itahakikisha makaa ya mawe yanakua chanzo kingine kikubwa cha
uzalishaji wa umeme nchini ili kupunguza gharama za umeme zilizopo hivi
sasa.
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameyasema hayo
alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka uliopo wilaya ya Mbinga
mkoani Ruvuma na kuongeza kuwa serikali itahakikisha inafanya kazi kwa
ushirikiano mkubwa na mgodi huo ili kuimarisha uchumi wa taifa kupitia
makaa ya mawe.
“Nimeelezwa
makaa ya Ngaka yana ubora na kiwango cha hali ya juu na nimeelezwa
kwamba kuna baadhi ya viwanda vimeingia mkataba na Ngaka lakini badala
yake wananunua makaa kutoka nje. Hilo halikubaliki ikiwa makaa ya ndani
ya nchi yana ubora lazima tutumie bidhaa za nyumbani,”amesisitiza Prof. Muhongo.
Kutokana
na malalamiko ya Mgodi kuhusu hali ya Mkataba ya kuuziana makaa
kutoafikiana, Waziri Muhongo ameutaka mgodi huo,Shirika la Maendeleo ya
Taifa (NDC),EWURA, Kampuni za Saruji za Dangote, Tanga Cement na Shirika
la Umeme Nchini (TANESCO) kukutana Makao Makuu ya Wizara tarehe 14
Januari,2016, ili kujadili kuhusu suala hilo na pia kujadiliana juu ya
gharama za kuuziana umeme na TANESCO pindi mgodi huo utakapoanza
kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Masoko wa mgodi wa Ngaka, Christopher Temba, mgodi
huo unazalisha tani za makaa ya mawe laki tano kwa mwaka na tayari makaa
hayo yanasafirishwa katika nchi za Kenya, Zambia, Malawi na vilevile
katika viwanda kadhaa hapa nchini vikiwemo vya Saruji, Mohamed
Enterprises na viwanda vingine.
Post a Comment