Featured

Loading...


Wema Hamjui Mwenye Mimba

wema.Wema Sepetu ‘Madam’
Na Mwandishi Wetu, Risasi
DAR ES SALAAM: Habari zinazosambaa kwa kasi ya ajabu kama moto wa kifuu zinaeleza kuwa, mtoto mzuri ndani ya Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ mbali na taarifa za kuwa mjamzito, hadi sasa bado yupo kwenye wakati mgumu kuweza kutegua kitendawili cha nani mmiliki halali wa kiumbe kilichopo tumboni mwake, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.
Hivi karibuni, magazeti tofauti ya Global Publishers ndiyo yalikuwa ya kwanza kuripoti kuhusu uwepo wa mimba ya mlimbwende huyo asiyechuja Bongo, ambapo awali, vyanzo mbalimbali vilieleza kuwa mhusika ni mbunge mmoja machachari ambaye ndiye anayemuweka Wema mjini kwa sasa.
WEMA 
Kitumbo cha Wema Sepetu
MAJIBU YA WEMA ALIPOBANWA
Kwenye habari ya awali iliyoripotiwa na gazeti la Ijumaa, Wema alipotafutwa kusomewa mashitaka yake kuwa ana ujauzito wa mbunge huyo, kupitia simu ya shosti wake, Aunt Ezekiel, staa huyo hakutaka kufunguka sana kuhusu mbunge huyo zaidi ya kusema; “ndiyo nina mimba, tena ya miezi sita.”
UBUYU MPYA SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Miss Tanzania  huyo wa mwaka 2006 amejiridhisha kuwa ni mjamzito baada ya kupima kwenye hospitali moja maarufu (jina tunalo) na kuondoka na furaha ya ajabu lakini kitendawili alichoondoka nacho ni kuwa hamjui mhusika wa kiumbe hicho.
WOTE AWAPA ASILIMIA 50
“Madam alifurahi kweli maana suala lililokuwa linamnyima usingizi siku zote ni kutopata mimba. Baada ya furaha hiyo, ishu ikawa ni kumtambua mhusika kwani kwa nyakati tofauti ameshabanjuka kimalavidavi na mshindi wa Big Brother Hot Shot 2014, Idris Sultan na mbunge yule anayempa jeuri ya pesa kwa sasa, wote amewapa asilimia hamsini hajajua nani hasa ndiyo mhusika,” kilisema chanzo hicho.
WOTE WAWILI KAWAMILIKISHA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baada ya kuona ameshachanganya madawa, Madam aliamua kila mmoja kumwambia kuwa ‘mzigo’ huo ni wake hivyo wote kwa pamoja na nyakati tofauti wanahudumia na kumjali staa huyo, tena kwa nguvu zote.
“Yaani kila mmoja kamwambia mimba yake. Wote wawili wamezipokea taarifa za ujauzito kwa bashasha huku kila mmoja akijiamini kuwa ni mhusika pasipo kujua Madam hajui nani hasa ndiye halisi.
MBUNGE, IDRISS ‘FULL’ KUHUDUMIA
“Yani ni full kuhudumia. Mbunge kwa wakati wake amekuwa akimwaga chapaa kama hana akili nzuri. Amelipia nyumba ile ya Ununio jijini Dar na kama hiyo haitoshi, amekuwa akisimamia shopping za maana tu mjini na hata ile ndiga aliyojizawadia Wema katika sherehe yake ya kuzaliwa, mbunge huyo alihusika katika malipo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Idris naye si haba. Anajitutumua kwa upande wake, anaamini kwamba mzigo ni wake bila kujua mimba hiyo ina figisufigisu.”
IDRIS ASAKWA, AFUNGUKA
Gazeti hili lilimtafuta Idris kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopokea, alitiririka hivi:
Risasi: Mzee tumepata habari kwamba wewe ndiyo mhusika wa mimba ya Madam, vipi unazungumziaje taarifa hizo?
Idris: Kwenye hilo kwa sasa siwezi kuliongelea, labda unipe mwezi mmoja. Kichwa changu hakijatulia.
Risasi: Lakini inasemekana unagharamia kila kitu kwa sasa, ukiamini mzigo ni wako?
Idris: Aaa! Acha kuniingizia hayo mambo bwana. Wewe subiri huo mwezi mmoja ukipita nitakueleza kila kitu.

SHOGA ZAKE WAMSHANGAA!
Mashosti wake waliozungumza na Gazeti hili ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ni jambo la kushangaza kwa mwanamke kushindwa kumjua mwanaume aliyempa ujauzito.

WEMA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kutosha kumsaka Wema kwa kumpigia simu na kumtumia ujumbe mfupi lakini hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
KUTOKA KWA MHARIRI
Mimba ni jambo la kheri hivyo kwa kuwa Wema ameziona simu za wanahabari wetu zikimuuliza juu ya mhusika wa kiumbe hicho, ni vyema akawapigia na kuanika kila kitu kuhusu habari hii.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top