Ndugu wasomaji,ni matumaini yetu kuwa mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya kila siku ikiwemo kufuatilia kampeni za wanasiasa ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi oktoba 2015.
Leo
napenda nizungumzie viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyojitokeza
katika kampeni za wanasiasa mbalimbali kuanzia ngazi ya madiwani,
wabunge na marais katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Kwanza
nianze kwa kuwapongeza wananchi kwa kuwa wavumilivu kutokana na kampeni
zinazoendelea hivisasa nchini za kushafuana, matusi, kejeli pamoja na
chama A kutuma wafuasi wavamie chama B au kuvuruga mikutano.
Watanzania
ni watu wavumilivu na wenye kupenda kuienzi amani tuliyoachiwa na Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa tuna amini kuwa
machafuko yakitokea hatuna pa kwenda pia tumejionea jinsi majirani zetu
na nchi nyingine wanavyopata shida yote haya ni kwa sababu ya machafuko
yanayosabaishwa na baadhi ya watu au kikundi fulani cha watu kwa maslahi
yao binafsi.
Aidha,Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndiyo iliyobeba dhamana ya kuangalia kama
kuna viashiria vya uvunjifu wa amani kwa wanasiasa katika kampeni zao
zinazo endelea hivisasa nchi Tanzania ikiwa ni siku 34 zimebaki kufikia
uchaguz mkuu unaodaiwa utakuwa wa Kihistoria tangu miaka 50 ya uhuru.
Kwa
mujibu wa maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa uachaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 kifungu cha 2.2 (a) Viongozi wa
Vyama vya Siasa, kinabainisha kuwa Wagombea hao hawatakiwi kufanya fujo
au kusababisha vurugu ya aina yoyote katika mkutano wa Chama kingine.
(b)
Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea wao hawatakiwi kutumia lugha ya
matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji na vitisho au lugha inayochochea
uvunjaji wa amani, au kuashiria ubaguzi wa kijinsia, ulemavu au
maumbile kwenye mikutano ya Kampeni.
Aidha,
Maadili hayo kifungu (c) kinaeleza kuwa mtu yeyote haruhusiwi kuwa
na/au kubeba silaha yoyote ikiwa ni pamoja na silaha za jadi au zana
yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika mkutano wa Kampeni au mkusanyiko
wowote wa kisiasa,na kifungu
(d)
kinaeleza kuwa hairuhusiwi kuwa na/au kubeba sanamu, kinyago au kitu
chochote ambacho kinaonyesha kudhalilisha, kukebehi au kufedhehesha
Chama kingine cha Siasa au Kiongozi wake au Serikali katika mkutano au
mkusanyiko wowote wa Kisiasa.
Licha
ya wanasiasa kuwa wanajua au wanapaswa kujua hivi vifungu vinasema
nini, wanasiasa hao wamekuwa wanakiuka maadili hayo kwa wazi kabisa kana
kwamba wapo juu ya kanuni na maadili ya NEC pasipo Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kuchukua hatua ikiwemo kukemea vikali viashiria hivyo vya
uvunjifu wa sheria husika, sheria zilizowekwa kwa madhumuni maalumu.
Wanasiasa wamekuwa wakitukana matusi hadharani ikiwemo Chama A kutukana chama B.
Lakini kinachoshangaza Tume ambayo tunasema inatakIwa itende haki na usawa kwa wanasiasa hao imekuwa ikiegemea chama kimoja au upande mmoja.
Lakini kinachoshangaza Tume ambayo tunasema inatakIwa itende haki na usawa kwa wanasiasa hao imekuwa ikiegemea chama kimoja au upande mmoja.
Nina
imani watanzania mtakubaliana na mimi kwamba kinacho endelea kwenye
kampeni za wanasiasa ni aibu hata kwa watoto kusikiliza kauli za
wanasiasa tunao dhani eti ndio watakuwa watawala wetu siku zijazo huku
wafuasi wao wakishangilia; najiuliza utu wetu uko wapi ?, je, huu ndio
uzalendo tunao sema kwa wanasiasa wetu?
Kwa
maoni yangu naomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi imulikwe ili iweze
kuchukua hatua kwa haraka kwani sisi wananchi wa kawaida machafuko
yakitokea hatutakuwa na pa kwenda kwa sababu wenzetu wanasiasa watapanda
ndege na kuelekea Ulaya wakati wananchi wa kawaida hatujui ata
Pasipoti ya kusafiria inafananaje na inapatikana wapi.
Wanasiasa wengi wamekuwa hawaelezi sera kwa wapiga kura, wamekuwa wakitukana Chama kingine au mgombea mwingine.
Kwa
mfano, Jana huko Chato,Geita Chama kimoja kati ya vyama vikubwa
kilifanya kampeni zake za kuomba ridhaa ya wananchi kuingia Ikulu.
Mmoja wa wanasiasa wazungumzaji alipopanda jukwaani alianza kumshambulia mgombea wa chama kingine huku akisahau kunadi sera za chama chake.
Mmoja wa wanasiasa wazungumzaji alipopanda jukwaani alianza kumshambulia mgombea wa chama kingine huku akisahau kunadi sera za chama chake.
Kilichonisikitisha
zaidi ni pale alipodiriki kusema mgombea huyo wa urais katika chama
Chenye nguvu kubwa hivisasa alijinyea akiwa stendi.
Sasa najaribu kujiuliza, kama ni kweli alijinyea;
1.Ni nani Alikizoa kile kinyesi?
2.Kuna ushahidi wowote unaoonyesha jinsi mgombea huyo alivyojinyea hadharani?
3.Hivi wafuasi wake wangekuwepo eneo hilo, amani ingetawala kweli?
Sasa najaribu kujiuliza, kama ni kweli alijinyea;
1.Ni nani Alikizoa kile kinyesi?
2.Kuna ushahidi wowote unaoonyesha jinsi mgombea huyo alivyojinyea hadharani?
3.Hivi wafuasi wake wangekuwepo eneo hilo, amani ingetawala kweli?
Badala
ya watendaji wa NEC kukaa maofisi tu, wangesambaza mawakala wao nchi
nzima kuangalia mienendo ya wanasiasa katika kampeni zao kwa maana ya
kufuatilia kwa karibu nini kinaendelea na kuchukua hatua endapo kuna
uvunjifu wowote wa sheria ikiwemo kampeni za matusi.
Post a Comment