
Dk.
John Magufuli leo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo
keshokutwa atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kutunuku kamisheni
kwa maofisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha (TMA),
Monduli.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, alisema Dk. Magufuli atawasili
kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na
amewaomba wananchi kujitokeza kumpokea.
"Nawaomba sana wananchi wa Mkoa wetu kwa mara ya kwanza tangu awe rais, ndio anakuja Mkoani kwetu, tujitokeze kumpokea,"alisema.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya
Kijeshi cha TMA Meja Jenerali PP Masao, Dk. Magufuli atatunuku
kamisheni kwa maofisa wanafunzi kundi la 57/15.
Alisema
Dk. Magufuli atatunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi kundi
hilo, katika sherehe zitakazoanza saa mbili asubuhi chuoni hapo.
Meja Jenerali Masao alisema wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.
Hii
ni ziara ya kwanza ya Rais Dk. Magufuli ambaye pia ni Amiri
jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, kufika mkoani Arusha
na pia kutunuku kamisheni, baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa
huo Oktoba, mwaka jana.
Post a Comment