Featured

Loading...


Walimu Wapigwa Marufuku Kupaka Wanja


Serikali wilayani Geita  Mkoa wa Geita, imepiga marufuku walimu kuvaa mavazi yasiyolingana na taaluma yao na upakaji wanja na rangi ya mdomo kupita kiasi wanapokuwa kazini.

Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Geita, Thabitha Bugema alitoa amri hiyo jana wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za msingi na waratibu elimu kwenye kikao cha muongozo wa kutumia fedha za elimu bure zilizotolewa na Serikali.

Bugema alisema baadhi ya walimu wanavaa mavazi ya upotoshaji ambayo hayaendani na ya ofisini.

Alisema walimu wa kiume huvaa suruali za jeans, fulana zenye nembo ya timu za mpira na wengine kuvaa mlegezo na kunyoa nywele mitindo isiyo ya heshima.

“Nashindwa kuelewa wapo walimu wanavaa kama wauza baa, amejipaka lipstick (rangi ya mdomo) na wanja kama anakwenda kwenye kumbi za muziki usiku, wakuu wa shule sitegemei kuwaona mkifumbia macho walimu wa aina hiyo,” alisema Bugema

Alisema kila mtumishi wa Serikali anafahamu mavazi ya ofisini na kuwataka walimu kubadilika na kuvaa mavazi ya heshima yanayoendana na taaluma yao.

Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Geita, Deus Seif alisema wamepokea Sh80 milioni kwa ajili ya elimu bure na kuwataka wakuu wa shule kuhakikisha zinatumika kama ilivyopangwa.

Mkuu wa wilaya hiyo, Manzie Mangochie aliwataka walimu na waratibu elimu kufanya mikutano ya wazazi ya kuwaelimisha maana ya elimu bure na kuwaeleza mambo ambayo Serikali inafanya na wajibu wa wazazi kwa watoto wao.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top