Featured

Loading...


Rose Ndauka Atoa Somo Kwa Wateja Wa DCB Commercial Bank Plc Katika Filamu Desire to Succeed

Rose Ndauka Atoa Somo Kwa Wateja Wa DCB Commercial Bank Plc Katika Filamu Desire to Succeed
Filamu ya Kuelimisha jamii Inayojulikana kama DESIRE TO SUCCEED (HAMU YA MAFANIKIO) kuzinduliwa Siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni 2015, Saa 12.00 Jioni katika ukumbi wa CENTURY CINEMAX Dar Free Market.
MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Rose Ndauka pamoja na wasanii wengine wakali katika tasnia ya filamu wameshiriki katika sinema maalum kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu huduma za Benki ya DCB Commercial Bank ambapo wateja wa Benki hiyo na wateja wapya watatambua huduma na faida zitokanazo na taasisi hiyo ya kifedha.
Rose Ndauka Atoa Somo Kwa Wateja Wa DCB Commercial Bank Plc Katika Filamu Desire to Succeed 2

Commercial Bank, ikishirikiana na Kampuni ya Consnet Group imeandaa Filamu maalumu ya Kiswahili inayoitwa DESIRE TO SUCCEED (HAMU YA MAFANIKIO) inayoelimisha na kuhamasisha wateja, wadau na umma kwa ujumla juu ya umuhimu na faida za kufanya shughuli za kibenki na DCB Commercial Bank ambazo zinabadili maisha ya mhusika.
Rose Ndauka Atoa Somo Kwa Wateja Wa DCB Commercial Bank Plc Katika Filamu Desire to Succeed 3
DCB Commercial Bank imeamua kuandaa Filamu hii baada ya kutambua kuwa Watanzania wengi wanapenda kuangalia filamu za Kiswahili na hivyo inaamini kuwa itaweza kuwafikia watu wengi na kufikisha ujumbe kirahisi zaidi.
“Tunashukru kwa Benki ya DCB Commercial Bank kutambua umhimu wa wasanii kushiriki katika kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu huduma bora zitolewazo na Benki hii, kuna wakati watu wanaogopa kujua huduma za kibenki kupitia filamu hii watafaidika sana,”anasema Rose Ndauka.
Moja ya changamoto zilizopo katika sekta ya benki ni jamii kukosa elimu ya kutosha juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya DCB na faida zake. Katika Filamu hii elimu, hamasa na faida mbalimbali za huduma za DCB Commercial Bank zimeonyeshwa.
Kadhalika Filamu hii inaelezea namna gani Account ya wanafunzi (DCB Student Acount) ilimsaidia Kijana Jensen kupata Elimu yake hata baada ya kufiwa na wazazi wake. Lakini pia ni namna gani baadaye kijana Jensen kwa kupitia account nyingine ya biashara (DCB Current Account) aliweza kupata mikopo ambayo ilimwezesha kufanya biashara zake kwa ufanisi na kupata faida kubwa na hivyo kuwa na msaada kwa wengine wenye shida ya fedha. Washiriki katika Filamu hii ni pamoja na Tito Zimbwe, Rose Ndauka, Jackline Pentezel, Abdul Mhema, HidayaNjaidi, Gojak na Wasanii wengine wengi.
Filamu hii itazinduliwa siku ya Jumamosi tarehe 25 June 2015, tunategemea mgeni rasmi kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa katika ukumbi wa Cinema wa Dar Free Zone kuanzia saa 12 jioni hadi saa 4 Usiku ambapo wateja wa DCB na wadau mbalimbali watakuwepo.
Baada ya kuzinduliwa Filamu hii itaonyeshwa katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dar Es Salaam yakiwemo City Center, Magomeni, Arnautoglu Mnazi Mmoja, Tabata, Temeke, Ukonga, Chanika, Mabibo and Kariakoo kuanzia tarehe 26 June 2015 hadi tarehe 14 Agusti 2015. Katika Uzinduzi rasmi DVD za filamu hii itauzwa kwa Shs 10,000. Filamu hii inasambazwa na kampuni ya Jasons Productions ya Jijini Dar Es Salaam. Kiingilio katika uzinduzi huo ni Bure.
Katika maeneo yote ambayo Filamu hii itaonyeshwa Wadau mbalimbali watapata nafasi ya kufungua akaunti mbalimbali zinazotolewa na DCB Commercial Bank kufuatana na mahitaji yao kama vile Akaunti za Biashara, Wanafunzi, Watoto, Akiba za watu binafsi, Vikundi, makampuni nk.
FC

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top