Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.
Profesa Makame Mbarawa wakati akijibu swali la nyongeza lililoihusu
Wizara yake ambapo ametaja maeneo ambayo mfumo huo utaanza kufanya kazi
ni pamoja na Mpanda mpaka Tabora, Kigoma mpaka Tabora.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani
akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Sabreen Hamza lililotaka
kujua kwanini TRL isianzishe mfumo wa uwakala wa tiketi ili kupunguza
adha wanayoipata wakazi alisema kuwa kutokana na mahitaji makubwa ya
usafiri wa treni katika Mikoa ya Kigoma, uuzaji wa tiketi katika
Stesheni ya Reli Kigoma umekuwa na changamoto kubwa kutokana na ulanguzi
wa tiketi.
Amefafanua
kuwa, ili kudhibiti ulanguzi huo, Kampuni ya Reli Tanzania iliamua
kubadilisha utaratibu kwa kuuza tiketi siku za safari na kwa kutumia
vitambulisho jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti
ulanguzi wa tiketi hizo.
Ameongeza
kuwa, utaratibu huo umekuwa na changamoto zake kwa kusababisha wasafiri
kulala stesheni au kuwalazimu kuamka alfajiri ili kuwahi tiketi hizo.
"Ufumbuzi
wa kudumu wa tatizo hili si kuanzisha mfumo wa uwakala ambao
utaiongezea TRL gharama za uendeshaji, tatizo kubwa lililopo ni idadi
ndogo ya safari za treni ambapo huduma inayotolewa hivi sasa haikidhi
mahitaji halisi ya wananchi na hivyo kuwa na uhaba wa tiketi kwa
abiria", alisema Mhe. Ngonyani.
Aliongeza
kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inatarajia kuongeza
idadi ya treni za abiria kwa njia ya Kigoma ili kukidhi mahitaji ya
wananchi wa Mkoa huo.
Post a Comment