Featured

Loading...


‘Wanaowatia Mimba Watoto Watungiwe sheria Kali’


SERIKALI imetakiwa kupunguza tatizo la kuwatia watoto wadogo mimba kwa kutunga sheria kali zitakazochukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya vitendo hivyo.
 
Kauli hiyo imetolewa jana na Diwani wa Kata ya Mnadani, Steven Masangia, katika kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kiwilaya ilifanyika Shule ya Sekondari Kikuyu B na kazi hiyo ilikwenda sambamba na watoto kupewa matone ya Vitamin A pamoja na dawa za minyoo.
 
“Serikali ina jukumu la kutunga sheria kali kwa wale wanaowatia watoto mimba kwani wamekuwa wakiwafanya washindwe kuendelea na masomo pamoja na kuwaharibia maisha yao ya baadaye,” alisema Masangia.
 
Masangia alisema ili kuwakinga watoto na janga hilo, ni muhimu kwao kukataa kukubali ofa wanazopewa za chipsi na zawadi ndogondogo kwa kuwa zimekuwa kichocheo cha kurubuniwa.
 
Diwani huyo alitoa wito kwa mashirika ya dini kulikemea jambo hilo kwa nguvu zote kwa kuwa halimpendezi hata Mungu.
 
“Niwaombe watoto mliopo hapa msikubali zawadi ndogondogo na chipsi kwani zimekuwa chanzo cha kutiwa mimba katika umri mdogo.
 
“Wazazi wana jukumu la kuhakikisha wanawapa elimu watoto hasa wale wenye ulemavu kwa kuweka miundombinu ambayo ni salama kwao,”alisema.
 
Masangia alitumia hotuba yake kukemea mauaji ya albino ambao alisema nao wana haki ya kuishi kama walivyo wengine.
 
Kwa upande wa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kikuyu B, Tatu Mohammed, aliitaka jamii kushirikiana ili kutokomeza tatizo la mimba za utotoni kwani kwa kufanya hivyo watapunguza magonjwa kama vistula.
 
Alisema tatizo lingine wanalokabiliana nalo ni watoto kuolewa katika umri mdogo hali inayochangia kupata magonjwa mengi kutokana na kutokomaa kwa nyonga.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top