Featured

Loading...


Tanesco Yazuia Shughuli za Kilimo Karibu na Nguzo


SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limetoa angalizo kwa wanaoendesha shughuli za kilimo, kwa kuwaambia hawatakiwi kulima karibu na nguzo kwani wanapaswa kuacha meta 30 kila upande.

Meneja wa Tanesco wa Mkoa wa Shinyanga, Mathias Solongo alitoa angalizo hilo kutokana na kuwapo malalamiko ya wananchi zaidi ya 50 wa kijiji cha Seseko kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga, dhidi ya Tanesco kuwakatia mazao.

Alisema wananchi hawaruhusiwi kulima sehemu zilizo karibu na nguzo za umeme ikizingatiwa kwamba, walishalipwa na manispaa hakuna sehemu ambayo haijalipwa.

“Na inayotakiwa kulipa ni manispaa siyo shirika na tayari ilishawalipa na katika nguzo hizo wananchi kweli hawatakiwi kulima, wanatakiwa kuacha mita 30 kila upande lakini tofauti ya hapo haitakiwi,” alisema.

Akizungumzia wananchi hao wanaolalamikia shirika, Solongo alishauri viongozi wa wananchi waende kwake azungumze na kuwaelewesha vizuri suala hilo.

Awali, wakizungumza na waandishi wa habari, wananchi hao wa kijiji cha Seseko, kata ya Mwamalili walisema miaka yote walikuwa wakiendelea kulima na hawakuwa na taarifa ya kuwakataza.

“Sisi tunachohitaji ni kulipwa mazao yetu yaliyokatwakatwa ambayo yamekatwa kimakosa kwani hata yakiiva hayafiki kwenye nguzo za umeme, baada ya hapo tulipwe fidia yetu ya ardhi kwani bado hatujalipwa. 
“Wamekata mtama wangu na mahindi yangu nitakula nini na watoto wangu, halafu wamekata bila hata kunitaarifu,” alisema William Deus.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top