Featured

Loading...


HUAWEI NA WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUUNGANA KATIKA KONGAMANO LA TEKNOHAMA NCHINI

Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk Ally Simba akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na kampuni ya Huawei katika kongamano la Teknohama, kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Samson Majwala.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Samson Majwala akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika kongamano la Teknohama. Kushoto ni Mkurugenzi wa ICT katika wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk Ally Simba.
Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk Ally Simba (Kushoto) wakishikana mkono na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Samson Majwala kuashilia kuungana katika kongamano la Teknohama.
Kampuni ya Huawei Tanzania ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Technolojia jana ilitangaza kuwepo kwa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference katika ukumbi wa Julius Nyerere Convential Center JNICC tarehe 18 na 19 Juni 2015.

Kongamano hilo litajadili hali ya sekta ya tecknohama kwa sasa,sera mpya zitakazowekwa na kuweka ajenda ya jinsi ya kukuza sekta hiyo nchini.pia kongamano hilo litaainisha jinsi nchi itafikia malengo yake ya milenia kupitia tecknohama.

Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Dk. Ally Simba alisema, “tumefurahi sana kwamba Wizara na kampuni ya Huawei Tanzania zitashirikiana katika kongamano hilo,ambapo tutajadiliana kwa undani ukuaji na maendeleo katika sekta ya ICT.Na kwa upande wa Wizara tutaelezea sera mpya na mipango tulioweka ili kuhakikisha maendeleo ya sekta”.

Aliendelea kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba Wizara imejikita katika kukuza sekta ya Teknohama.aliongeza kwamba Makamo wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anategemewa kuwa mgeni rasmi,huku pia ,Waziri na Katibu Mkuu wa Wizaraya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia na Balozi wa China nchini Tanzania watakuwepo.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Bwana Samson Majwala alisema, “tunaishukuru sana Wizara kwa kukubali kuungana nasi katika kuandaa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference nchini Tanzania,na tunawahakikishia Watanzania wote kwamba kongamano litapendeza.Tutakua na wataalam kutoka nyanja tofauti za Teknohama kutoka serikalini na kampuni ya Huawei ambao watatuelimisha kuhusu mitindo mipya katika sekta hiyo.Sisi kama Huawei tutaelezea mipango tuliyonayo ya kuboresha sekta hii nnchini Tanzania”.

Katika kongamano hilo,Huawei watazindua bidhaa zao mpya za Oceanstor V3 na Fusonq.Pia kutakua na gari maalumu la kufanya maonesho,gari hilo kwa kila mwaka linafanya ziara katika mabara yote duniani,na kwa mwaka wa 2015 litazuru bara la Afrika haswa Afrika kusini na Afrika Mashariki,Tanzania ikiwemo ya nchi itakayopita.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top