Featured

Loading...


SUMAYE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS 2015

Sehemu iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea urais katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye akitangaza nia ya kugombea urais mbele ya wananchi waliohudhuria mkutano huo leo.
Meza kuu, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Ester Sumaye (kushoto) Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (katika) Mwenyekiti wa UVCCM wa Kinondoni, Shabani Uronu, pamoja na Katibu Mwenezi CCM, Kata ya Kiluvya, Juma Semindu.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria kusikiliza mkutano huo.
Sehemu ya wanahabari waliopata fursa ya kuuliza maswali mmoja wao akiuliza swali.
Mhe.Sumaye (katikati) akitafakari kujibu swali aliloulizwa na mwanahabari (hayupo pichani).
Mhe.Suamaye alipokuwa akiingia ndani kwa ajili ya kutoa tamko la kutangaza nia ya kugombea urais .
Wananchi wakipepea bendera baada ya kumaliza kutangaza nia ya kugombea urais .
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Tluway Sumaye leo ametangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania kwa mwaka wa 2015 kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza leo mbele ya wananchi na wanahabari katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro Hoteli) jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema kuwa ameamua kutangaza nia ya kuwa mgombea urais kutokana na alivyoweza kujipima mwenyewe, kujishauri na kutafuta ushauri kutoka kwa watu wengine na kuona kweli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema kuwa amejitathimini na kuona kuwa yeye ndiye anayetosheleza kuwa kiongozi wa nchi hii kutokana na jinsi alivyoweza kuongoza nchi hii akiwa Waziri Mkuu kwa zaidi ya miaka 9 na hivyo  anastahili kuiongoza nchi.
Aliongeza kuwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika utumishi wa umma, kama ubunge, unaibu waziri, Uwaziri na hatimaye kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
 “Katika uongozi wangua nilijitahidi sana kusimamia uchumi wa taifa kama vile, kusimamia uchumi, kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliyokuwa ikiongoza kwa uchafu wa mazingira miaka ya 1996, kutengeneza madawati kwa shule zote za msingi, kuweka televisheni ya taifa, mpango wa maendeleo Elimu (MMEM) na mambo mengine, ”alisema.
Vilevile alieleza juu ya kufanya kazi kwa muda huo wote katika ngazi mbalimbali kuwa ni dhahiri nchi anaifahamu pamoja na shida za wananchi pamoja na  matatizo yao anayajua, kila eneo na kila kanda hivyo akiteuliwa kuwa rais hatahitaji kujifunza juu ya nchi ya Tanzania.
Wakati akizidi kufafanua alieleza malengo yake endapo akiteuliwa kuwa rais kuwa lazima atazingatia mambo yafuatayo ili kuweka uchumi imara katika nchi yetu ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kulinda muungano pamoja na amani na utulivu, kuimarisha uchumi, kupambana na maovu ya rushwa kama vile ufisadi na madawa ya kulevya na mauaji, kuboresha huduma za jamii na ajira pamoja na michezo.
Waziri Mkuu Mstaafu alipoulizwa swali juu ya ambao wote tayari wamekwisha tangaza nia ya kugombea urais kwa mwaka 2015 kuwa nani anamwona kuwa kinara zaidi yake  alisema kuwa yeye ndiye anafaa kuwa kiongozi wa nchii hii kwani wote waliokwisha tangaza haoni kama wana imani na kuongoza nchi yetu.
PICHA/STORI: DENIS MTIMA/GPL

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top