Hakika Mungu ni mwema sana. Ametuwezesha leo kuwa na nguvu ya kutafakari hatima ya nchi yetu ambayo inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 hapo Oktoba.
Mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakijitokeza kuwania urais kupitia chama hicho na tayari wameanza kuchuana kutangaza nia yao baada ya vikao vya Kamati Kuu Taifa (CC) na Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kumalizika hivi karibuni mjini Dodoma na kutoa baraka zote kuanza rasmi kwa mchakato huo.
Ninachowaomba watangaza nia ni kwamba wasitumie mwanya huo wa kujitangaza kuchafua wenzao na badala yake wajenge hoja bila kupitiliza kwa sababu kampeni rasmi zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi bado hazijaanza.
Kila mtangaza nia anatakiwa ajipange kuwaeleza Watanzania jinsi ya kuboresha maisha duni ya wananchi kwani walio wengi ni magumu.
Watangaza nia wajipange kueleza jinsi ya kuondoa mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali nchini ambao uko juu, wajipange kueleza wataisaidiaje jamii?
Niwaase watangaza nia hasa kutoka chama tawala CCM kwamba kila neno watakalokuwa wanalitamka litakuwa linapimwa na wananchi.
Niwaase watangaza nia hasa kutoka chama tawala CCM kwamba kila neno watakalokuwa wanalitamka litakuwa linapimwa na wananchi.
Kwa hiyo basi, watangaza nia watakaotumia majukwaa kuwachafua wenzao, moja kwa moja watakuwa wamekwenda ‘nje ya reli’ kwa sababu sasa hivi wananchi wanataka kiongozi ambaye ataeleza jinsi ya kuwakwamuwa kiuchumi, kimatibabu na kielimu.
Ni jambo la msingi sasa kwa wana CCM kupima wagombea wao na wasijazane tu kwenye mikutano ya kutangaza nia na kushangilia kishabiki bila kupima neno kwa neno.
Post a Comment