Featured

Loading...


Wagombea Urais CCM Wakimbia Mdahalo Dar

Mwenyekiti wa Mdahalo, Ally Mfuruki

WAGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), juzi walikimbia mdahalo wa kupambana kwa hoja ulioandaliwa na wenyeviti wa sekta binafsi na kujulikana kama ‘CEO round table of Tanzania’.
 
Mdahalo huo ulikuwa na lengo la kujadili mambo makuu mawili, ikiwa ni sekta ya uchumi na utawala bora na kwa jinsi gani wagombea hao wakipata ridhaa ya kuliongoza taifa, wangetekeleza vipaumbele hivyo katika kuliletea taifa maendeleo.
 
Akizungumza mara baada ya kuahirisha mdahalo huo, Mwenyekiti wa Mdahalo, Ally Mfuruki alisema amesikitishwa sana na wagombea hao kwa kushindwa kuhudhuria kwenye mdahalo huo, kwani hadi muda unakaribia wa kuanza majadiliano, walitoa taarifa za kuhudhuria.
 
“Nashindwa hata kuelewa ni sababu zipi zimewafanya hawa wagombea wasifike kwani muda mfupi tu uliopita niliwasiliana nao na wakasema wanakuja, lakini baada ya kuona muda unaenda na hakuna aliyefika, nikapata taarifa kuwa hawatafika na sijapewa ni sababu zipi zimewakwamisha,” alisema Mfuruki.
 
Waliotarajiwa kuhudhuria mdahalo huo ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Mawasiliano January Makamba, Balozi Amina Ally, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
 
Alisema anashangaa kutojitokeza kwao na kuwa aliyejitokeza ni mgombea mmoja tu, mwanamke pekee katika kinyang’anyiro hicho cha kuwania kiti cha urais, ambaye ni Balozi Amina Ally.
 
Lakini, alithibitisha kupokea taarifa za kutohudhuria kwa Waziri Nyalandu na kusema kuwa alipata dharura ya kikazi na hivyo alitoa taarifa ya kutohudhuria mapema na Sumaye pia alipata dharura na kutoa taarifa ya kutokuwepo kwenye mdahalo.
 
Kwa upande wake, Balozi Amina Ally alisema anasikitishwa na wagombea wenzake kwa kutoitika wito wa kuhudhuria, kwani wananchi wanachokitaka ni kuwafahamu kwa undani wagombea kwa kupitia midahalo na kuweza kutambua ni yupi atakayewaletea maendeleo na kuwatatulia changamoto zinazowakabili.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top