Featured

Loading...


Dkt Kikwete atunukiwa Shahada ya Heshima ya Kimataifa Katika Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT)


Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa jana Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.

Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa Shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo katika jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.

“Naipokea heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe. Dkt  Kikwete.

Mbali na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali duniani waliwahi kupata Shahada za heshima toka Chuo Kikuu Huria Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Hayati  Nelson Mandela na Dkt Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa UNESCO.

Chuo kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla ya wahitimu 69 wawili Shahada maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na Astashahada, ambapo Shahada ya uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya uzamili ni wahitimu 20, Shahada wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na Astashahada wahitimu 6.

Tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria Tanzania mwaka 1992 jumla ya wahitimu 25,908 wametunukiwa Shahada mbalimbali na haya ni mahafali ya 30 tangu chuo   kuanzishwa
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimpongeza Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku Shahada  ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa katika  maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika jana Jijini  Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanataaluma na wageni katika  maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika jana Jijini  Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akifungua rasmi mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika  jana Jijini Dar es Salaam

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright 2025 JICHO LETU | Designed By Code Nirvana
Back To Top