Featured

Loading...


Mbunge aitaka Serikali ianzishe idara ya vipodozi


MBUNGE wa Mji Mkongwe, Ibrahim Sanya (Chadema), ameitaka Serikali kuanzisha elimu ya madhara ya vipodozi visivyo na viwango kwa shule za msingi.
 
Akiuliza swali bungeni jana, Sanya alisema kuanzishwa kwa elimu hiyo kunatokana na Serikali kushindwa kudhibiti uingizwaji wa vipodozi hivyo  nchini hali inayosababisha kuogezeka kwa matumizi.
 
“Kwa nini Serikali isishirikiane na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuingiza elimu ya madhara ya vipodozi katika somo la sayansi ili wanafunzi wa shule za msingi wajue madhara yake ikiwemo kuonyeshwa picha za watu walioathirika?” alihoji.
 
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe alisema progamu ya kufundisha madhara ya vipodozi kwa shule za msingi imeshaanza tangu mwaka 2009.
 
Awali akijibu swali la msingi la Sanya, Dk. Kebwe alisema Wizara yake kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imeweka utaratibu wa kudhibiti uingizaji na utoaji nje ya nchi wa vipodozi pamoja na bidhaa nyingine inazozidhibiti.
 
“Hadi sasa jumla ya vipodozi 2,527 ndivyo vimeruhusiwa kuingizwa nchini.
 
“Vilevile katika mwaka wa fedha 2014/15 mabasi ya abiria matatu yalikamatwa mkoani Mbeya na Dar eas Salaam yakiwa yamebeba vipodozi ambavyo havijasajiliwa kutoka nchi jirani na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
“Katika mwaka 2014/15, jumla ya tani 16.61 za vipodozi vilivyopigwa marufuku vyenye thamani ya Sh. milioni44.2 zimeteketezwa na TFDA,” alisema Dk. Kebwe.
 
Alisema elimu imekuwa ikitolewa njuu ya matumizi sahihi ya vipodozi na kwamba mwaka 2014/15 shule 16 zilitembelewa na elimu kutolewa juu ya matumizi ya vipodozi.
 
Katika swali lake Sanya alitaka kujua lini Serikali itakuwa makini kuzuia vipodozi ambavyo havina viwango kuingia nchini.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top