Featured

Loading...


ULIMWENGU HUU WA WAPENDANAO KILA MTU AMEJERUHIWA, UTAISHIJE?

NIANZE kwa kumshukuru Mungu kwa kunikutanisha na wewe Jumamosi nyingine tulivu. Kama kawaida, mimi na wewe tunakutana kuweza kupeana darasa la uhusiano wa kimapenzi.
Nitoe shukrani za dhati kabisa kwa wale walionitumia ujumbe mfupi wa maneno kuonesha waliguswa na mada ya wiki iliyopita iliyokuwa ikielekeza namna ya kumjua mchumba wako kama ana mapenzi ya dhati. Asanteni na tuendelee kujifunza.
Bila kupoteza muda leo tuzungumzie mada iliyopo mezani. Ni ukweli usiopingika kwamba katika kizazi hiki cha sasa watu wengi sana wamejeruhiwa. Ukimuuliza kila mtu historia yake ya mapenzi atakwambia ameshajeruhiwa sana.
Atakwambia ameshaumia vya kutosha. Atakwambia imefika wakati haoni hata umuhimu wa kupenda tena. Anapoteza kabisa hamu ya mapenzi. Haamini kama kuna watu wanaofurahia mapenzi.
Atasema hivyo kwa sababu, aliumizwa na mpenzi wake wa kwanza, akampata wa pili mambo yakawa yaleyale, wa tatu ndiyo usiseme na wa nne ndiyo kabisa.Hili ni tatizo kubwa. Mtu anakuwa amependa kiasi ambacho anajisahau kabisa kama mwenzake anaweza kumtenda wakati wowote, ghafla anajikuta ameachwa.
Madhara ya kujeruhiwa siku zote ni makubwa, unakosa msimamo. Leo utaonekana na huyu kesho utakuwa na mwingine. Mbaya zaidi umri nao unakuwa si rafiki kwako. Licha ya kuwa tatizo hili pia linawagusa wanaume lakini kwa wanawake huwa ni mara dufu.
Mwanaume anaweza kujeruhiwa kwa muda mrefu lakini umri ukaendelea kuwa rafiki kwake. Anaweza kuoa binti mdogo bila kujali umri wake. Kwa mwanamke ni ngumu kidogo wanaume wengi wanataka kumuoa mwanamke ambaye hajazeeka. Hiyo ndiyo sababu ya kimaumbile.
Kwa mwanamke ina madhara makubwa zaidi. Umri unakuwa kigezo kikubwa cha kupoteza sifa kwa wanaume, matokeo yake anapoteza matumaini ya kuishi katika ndoa. Kuolewa kwake inakuwa ni nadra, hapo ndipo linapokuja suala la ‘acha na mimi nizae tu niache kopi yangu duniani.’
Haijalishi atazaa na nani, anazaa kwa sababu ameshapotea dira ya kuolewa. Anachokiangalia kwa wakati huo ni kupata mtoto ili na yeye aitwe mama.Ili kuzidi kujifunza, tusome pamoja mfano huu wa mama aliyenitumia ujumbe mfupi akiniomba ushauri:
“Anko samahani, mimi ni mama wa watoto wawili. Nimepata maumivu makubwa ya kimapenzi. Kila mwanaume ambaye nimeanzisha naye uhusiano, amenitenda. Nilipata bahati mmoja tuliishi naye, nikapata ujauzito, nikajifungua. Baada tu ya kujifungua akaanza kubadilika. Kwa kuwa na mimi nilianza kupoteza imani naye, akaanza kunitoka moyoni.
“Bahati mbaya au nzuri tena nikapata mimba yake nyingine, nikajifungua. Visa vikazidi kuongezeka, akanifanyia vitimbi vya kila aina na kudai hataki hata kuniona. Ilifika wakati aliniletea hadi mwanamke mwenzangu ndani. Kama hiyo haitoshi alianza hadi kusema eti watoto niliozaa naye si wake, nisimjue. Nikaamua kuachana naye, nikaondoka na kwenda kuishi kivyangu, umri umekwenda anko, sina imani na kila mwanaume nifanye nini?”
Kupitia mfano huo tunajifunza kwamba kunahitajika umakini wa hali ya juu katika kuamua kuanzisha uhusiano na mtu. Muombe sana Mungu akusaidie kukutanisha na mtu sahihi kwako. Kabla ya kufikia kufanya maamuzi ya kubeba ujauzito hakikisha mtu huyo amekuridhisha katika kila eneo.
Mchunguze mtu ujue historia na tabia yake. Tabia ya mtu huwa haiwezi kujificha kwa muda mrefu. Kupitia matendo yake katika kipindi cha kumchunguza utamjua ni mtu wa aina gani. Mpe nafasi ya kuzaa naye pale tu utakapokuwa umeridhika na sifa zake.
Ukiishi naye kwa kipindi kirefu cha uchumba, akafuata taratibu zote na ikiwezekana mzae wakati mmeshafunga ndoa.
Ikiwa imetokea umeshazalishwa, ishi kama haujawahi kutendwa. Jitahidi kujipa furaha kadiri uwezavyo, muombe Mungu atakupa mtu sahihi ambaye ataridhia, atakupenda kwa hali yoyote!
Licha ya kukupenda wewe, atawapenda wazazi, ndugu na marafiki zako.
Nasema hivyo kwa sababu hicho pia ni kigezo ambacho mtu aliyekupenda anapaswa kuwa nacho.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top