Karibu katika muendelezo wa mada yetu tuliyoanza wiki iliyopita, mada yetu inajieleza hapo juu.Tulijifunza wiki iliyopita kabla ya kutafuta atakayekufaa na kukupenda, wewe binafsi unapaswa kufanya yafuatayo;

Jiepushe na makundi
Umri wa kijana ndiyo pekee wenye changamoto nyingi sana katika uso wa dunia kama vile ; vishawaishi, tamaa, majaribu na mengineyo. Kama kijana unapaswa uchague watu wa kuwa nao usipende kufuata mkumbo kwa sababu John au Juma wanafanya kitu flani basi na wewe unaiga. Tabia ya kuiga ni kukosa kujiamini kama kijana, jaribu kuwa wa kitofauti, siyo kila kitu huigwa, vingine hupuuzwa pia.

Jichunguze
Unapaswa ujichunguze kwa makini, wewe ni wa thamani kiasi gani? Na mwisho ujue wewe si wa kila mtu anayetaka kupumzika na kujistarehesha basi anapumzikia kwako.

Jiheshimu
Lazima ujiheshimu kwanza wewe na wengine watakuheshimu tu bila kujali kipato, elimu au jinsia yako, lakini kama utakuwa waluwalu kila mtu akikutaka anakupata, asipite msichana yeyote mbele yako unaye hilo ni tatizo.

Jitathmini
Je, ni vitu gani vitamfanya mwanamke au mwanaume aweze kuwa mwenza wako, je ni tabia yako nzuri au mbaya? Ni tabia yako ya roho mbaya au upendo? Uzinzi na uongo au uchoyo na ushirikina?

Bidii katika maombi
Swala la ibada ni jambo muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu, kila muda na kila mahali, si tu mpaka wakati wa matatizo. Vijana wengi wa Kikiristo wamesahau kuwa ‘Kumcha Mungu ndiyo chanzo cha maarifa,’ mke mwema anatoka kwa Mungu, hata vijana wa Kiislam nao wamesahau kuwa ‘Allah akbar ‘(Mungu mkubwa).

Kama vijana watatumia nguvu, akili na muda wao mwingi katika kumtukuza Mungu kwa sala, kufunga na maombi inawezekana kukupa mtu anayefaa kama mumeo au mkeo.
Tukutane wiki ijayo katika mada nyingine nzuri.

Post a Comment