Featured

Loading...


RUNGWE MAGHARIBI; SOKO LA MAZAO, HUDUMA ZA KIJAMII BADO NI TATIZO

Rungwe ni moja kati ya wilaya nane zinazounda Mkoa wa Mbeya. Upande wa Kaskazini imepakana na Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mashariki imepakana na Mkoa wa Iringa na Wilaya ya Kyela, Kusini Magharibi kuna Wilaya ya Ileje na Magharibi kuna Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Profesa David Mwakyusa.
Wilaya ya Rungwe, imeganyika katika majimbo mawili ya uchaguzi, Rungwe Magharibi linaloongozwa na Profesa David Mwakyusa na Rungwe Mashariki linaloongozwa na Profesa Mark Mwandosya.
Wiki iliyopita, Gazeti la Uwazi lilifanya ziara kwenye jimbo la Rungwe Magharibi na kuzungumza na wananchi walioeleza matatizo yanayowakabili na jinsi mbunge wao anavyozishughulia kero mbalimbali zinazowakabili.
MATATIZO YA WANANCHI
Katika ziara yake jimboni humo, mwandishi wetu alikumbana na malalamiko ya wananchi wa Kata ya Masomo ambao wanalalamikia kukamilishwa kwa mradi wa maji wa Masoko ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2012, hali inayosababisha waendelee kuteseka kwa kukosa maji safi na salama, wakati mwingine wakikumbwa na magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara kutokana na kunywa maji machafu.
“Hawa viongozi wa serikali wanakula hela tu, mradi gani tangu mwaka 2012 mpaka leo haujakamilika? Huu ni ufisadi wa waziwazi,” alisema Anania Mwasomola, mkazi wa Masoko jimboni humo.Tatizo lingine ambalo Uwazi lilibaini, ni ukosefu wa bei nzuri za mazao ya wakulima. Wananchi wengi wa Rungwe Magharibi wanajishughulisha na kilimo cha ndizi, kahawa na chai.
“Kwa kweli sisi wakulima tunapata sana shida, bei ya chai siyo ya kuridhisha, tunatumia muda mrefu na gharama kubwa kuhudumia chai lakini bei tunayouzia kwa kweli inakatisha sana tamaa.“Upande wa ndizi ndiyo kunachosha kabisa, wachuuzi kutoka mjini wanakuja kununua ndizi kwa bei ya chini halafu wao wanaenda kuuza Dar kwa bei kubwa na kutuacha sisi tunaendelea kuwa maskini. Tunaomba serikali itusaidie,” Gabriel Mwakajwanga, mkazi wa Lufingo aliliambia Uwazi.
Matatizo mengina ambayo yamelalamikiwa na wananchi wengi wa jimbo hilo, ni ukosefu wa viwanda vya kusindikia mbogamboga na matunda yanayozaliswa kwa wingi jimboni humo, jambo linalosababisha wakulima waendelee kuogelea kwenye dimbwi la ufukara.
“Kwa mfano mimi nina shamba langu la miparachichi inayowahi kutoa matunda na kukomaa haraka, nilipata mbegu kutoka Chuo cha Kilimo Uyole. Cha ajabu ni kwamba nazalisha maparachichi mengi lakini hakuna soko la uhakika, mengine yanaharibikia shambani.
“Kama serikali imeshindwa kututafutia soko basi watujengee hata viwanda vya kusindika hukuhuku kwetu,” Enock Mwakalinga aliliambia Uwazi.Uhaba wa dawa, vifaa vya tiba na wauguzi kwenye hospitali nyingi jimboni humo ni tatizo jingine lililoelezwa na wananchi wa jimbo hilo, sambamba na uhaba wa madawati, michango ya mara kwa mara na uhaba wa walimu kwenye shule nyingi za kata jimboni humo.
Ubovu wa miundombinu, tatizo la utoro kwa wanafunzi wa kike mashuleni ambapo wengi huolewa wakiwa na umri mdogo, ni matatizo mengine ambayo Uwazi liliyabaini katika ziara hiyo.
MAELEZO YA MBUNGE
Baada ya kusikia upande wa wananchi, Uwazi lilihamia upande wa mheshimiwa mbunge wa jimbo hilo kutaka kusikia anazungumziaje kero za wananchi wake. Baada ya kumtafuta ana kwa ana bila mafanikio, lilifanikiwa kumpata hewani kwa kupitia simu yake ya kiganjani ambapo mwandishi wetu alipojitambulisha, aliomba atumiwe ujumbe mfupi kwa sababu alikuwa kwenye mkutano.
Mwandishi wetu alimtumia ujumbe unaoeleza kero zote za wananchi lakini mpaka gazeti linakwenda mitamboni, mheshimiwa huyo hakuwa amejibu chochote. Jitihada zinaendelea ili atoe ufafanuzi wa matatizo yanayowakabili wapiga kura wake, bado zinaendelea.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top