Staa wa bongo movies, Halima Yahaya ‘Davina’ amekiri kuwa makundi huwa yanaharibu watu walio kwenye ndoa kwa kuwalaghai kwamba wakaonje nje kwa lengo la kuangalia radha nyingine hali amabayo wakati mwingine mawazo hayo humjia lakini ghafla huhisi kama mumewe atamuona na kuhatarisha ndoa yake.
Akizungimza na Tanuru la Filamu , Davina alisema kwamba alipata wakati mgumu wakati wakuigiza filamu ya SHANTA inayotarajiwa kuingia sokoni wiki hii ambayo alicheza kama mke wa mtu ambaye alichepiuka na mwanaume na wakati anatoka gesti akafumaniwa na mumewe.
“Kweli wakati mwingine mawazo kama haya huwa yanakuja unaposikiliza stori za wanawake wachepukaji lakini huwa nafikiri nifanye hivyo kwa kukosa nini kwa mume wangu?
"Kutokana na msimamo huo nilipata tabu kuigiza filamu ya SHANTA ambapo niliigiza kama nimemsaliti mume wangu na kweli kwenye filamu hiyo nilifumaniwa , inakera sana wanandoa kusalitiana,” alisema staa huyo.

Davina alisema filamu hoyo itasambazwa na kampuni ya 5 Effects Movies Ltd na anaamini itawafundisha watu wengi ambao wamekuwa wakishindwa kutulia kwenye ndoa zao ambapo mwisho wa siku huambulia kuambukizana magonjwa.
Post a Comment