Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI Hamis Kiiza raia wa Uganda, jana alitua nchini kwa ajili ya kufanya mchakato wa kumalizana na Simba, ambapo kauli aliyotoa na maandalizi ya Simba, vimeonyesha kuwa pande zote mbili hazina utani katika kujiandaa na msimu ujao wa 2015/2016.
MSHAMBULIAJI Hamis Kiiza raia wa Uganda, jana alitua nchini kwa ajili ya kufanya mchakato wa kumalizana na Simba, ambapo kauli aliyotoa na maandalizi ya Simba, vimeonyesha kuwa pande zote mbili hazina utani katika kujiandaa na msimu ujao wa 2015/2016.
Simba ambayo imeshaweka wazi kuhusu kumsajili Kiiza aliyekuwa akiitumikia Yanga kwa miaka kadhaa, imeelezwa kuwa anatarajiwa kukabidhiwa nyumba ya kuishi maeneo ya Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Kiiza aliyepokelewa na mchezaji wa zamani wa Simba, Poffen Martine, alitamka kuwa amekuja Tanzania kufanya kazi.
“Nimekuja kwa ajili ya kufanya kazi, sina tatizo na Yanga kwa kuwa niliondoka kwa amani, nafurahi kurejea tena Bongo kwa kuwa najua nikimalizana na Simba litakuwa jambo zuri kwangu na kwa klabu.
“Ushirikiano wangu na wachezaji wengine akiwemo (Emmanuel) Okwi naamini utakuwa na faida kwa kuwa tunajuana vizuri na sote ni watu wa kazi,” alisema Kiiza aliyekuwa ameongozana na mchezaji mwingine wa Simba, Simon Sserunkuma.
Mara baada ya kutua uwanjani hapo, Simon alizungumza na simu kisha akamwambia Kiiza wanatakiwa kuelekea ofisini moja kwa moja bila kufafanua ni wapi, lakini gazeti hili lilipata taarifa kuwa wanaelekea kuonana na Rais wa Simba, Evans Aveva.
“Nawaonea huruma mashabiki wa Yanga kwa kuwa najua watakuwa wanajisikia vibaya lakini mimi nipo kazini na soka ndiyo ajira yangu,” alisema Kiiza ambaye pia amekuwa akifanya vizuri anapocheza na Okwi katika timu ya taifa ya Uganda.
Akimzungumzia Kiiza, Simon alisema: “Naamini Simba imepata jembe la ukweli kwa kuwa Kiiza ni mchezaji wa kiwango cha juu na najua atakuwa na msaada mkubwa klabuni.”
Aidha, chanzo kutoka Simba kimefunguka kuwa, Kiiza atapangiwa nyumba hiyo kisha kuishi pamoja na wachezaji wenzake wa kigeni ili kuzoea mazingira kabla ya kuanza ujenzi wa hosteli ya klabu katika uwanja wao, ambapo wachezaji wote watahamia huko.
“Kuhusu (Laudit) Mavugo, atatua siku yoyote kuanzia sasa kwa kuwa yupo katika hatua za mwisho za mazungumzo na viongozi,” kilisema chanzo hicho.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Collin Frisch, alisema Kiiza atafanyiwa vipimo vya afya kisha michakato itaendelea bila kufafanua.
Post a Comment