Featured

Loading...


MASTAA BONGO WANAVYOUTENDEA HAKI MFUNGO WA RAMADHANI!

   Na Hamida Hassan
Kila unapofika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mastaa wengi Bongo hubadili mienendo yao kimavazi na hata matembezi, haijalishi kuwa wote ni waumini wa Dini ya Kiislamu au wa Kikristo, wote hujikuta wameungana na kuwa kitu kimoja.
MAVAZI
Baadhi ya mastaa hao hujikuta wanavaa mavazi yanayofanana kwa maana ya kuuheshimu mwezi huu na kuutendea haki. Huvaa nguo ndefu na wengi hujistiri kwa kuvaa vitambaa na mitandio kichwani.
Ukizungumza na baadhi ya mastaa wanakuambia mwezi huu huwa ni mwezi wa kuheshimiwa, haijalishi ni Muislamu au Mkristo ndiyo maana huungana na kuwa kitu kimoja.
FUTARI
Mara nyingi utakuta mastaa wanaamua kuungana hata kwenye kuandaa futari na kula kwa pamoja bila kujali dini, kwani Wakristo na Waislamu hukutana kwenye mlo na kufurahia pamoja ikiwa ni sambamba na kuomba dua ya pamoja. Hakika hupendeza na si rahisi kutambua tofauti ya dini ya mwingine.
MASTAA WAKRISTO WANAOJISITIRI!
Baadhi ya mastaa Wakristo ambao hupendelea kufunga na kuvaa mavazi yanayostiri miili yao sambamba na Waislamu ni pamoja na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’, Waigizaji Vanitha Omary, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Devotha Mbaga, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula,’ Elizabeth Michael ‘Lulu’, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mastaa wa Bongo Fleva, Pamela Dafa ‘Pam D’ na Estalina Sanga ‘Linah’.
WAISLAMU WANAOBADILI MAVAZI
Kuna baadhi ya mastaa ambao hupendelea kujiachia kwa vimini na nguo tata lakini kwa mwezi huu wamebadili mavazi kama waigizaji Aunt Ezekiel, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Wema Isaac Sepetu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Halima Haroun ‘Kimwana’, Snura Mushi, Shamsa Ford, Halima Yahya ‘Davina’, Rose Ndauka, Sabrina Rupia ‘Cathy’ na wengine wengi.
Kwa harakaharaka anayekutana na mastaa hawa mwezi huu na kutangaza ndoa, anaweza kujikuta anajuta kwani mwezi ukiisha mavazi hayo huwa yanafungiwa kabatini na kusubiri mwezi mwingine au msiba kwani huamua kurudi kwenye vivazi vyao ambavyo naweza kuviita ni vya asili yao kwani karibu wote wamejikuta wakipendelea kuvaa hivyo.
Je, kuwa staa ni lazima uvae nusu utupu? Hili ni swali ambalo huwa najiuliza kila siku lakini nawaombea mastaa wetu siku moja wabadilike.
Kwa nini isitokee mavazi haya ya nusu utupu yakavaliwa pale inapobidi tu, nikisema hivyo namaanisha kwenye kazi tu kwani tunajua kuna kazi ya staa ambayo inamlazimu kuvaa nusu utupu lakini si kuyafanya ndiyo mavazi rasmi ya kila siku.





J

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top