Featured

Loading...


NI AIBU KUWA MPOKEAJI TU WA ZAWADI ZA MPENZI!

Awali ya yote niwapongeze wale ambao wanaendelea na mfungo. Ni jambo la heri kulifanya kwani faida yake inajulikana. Kwa sisi tulio kwenye mapenzi ya kawaida (ambao hatujaoana) ni kipindi cha kuwa makini sana kuhakikisha hatutibuliani.
Kama uko kwenye uhusiano na mpenzi ambaye ni Muislamu, heshimu imani yake kwa kuhakikisha humuwekei mazingira ya kumharibia swaumu kama vile kulazimisha kukutana naye faragha, kumtumia sms za kimapenzi au kumtaka mtoke ‘out’ na kwenda sehemu ambazo hazifai.
Hayo ni kati ya mambo ambayo mnatakiwa kujiepusha nayo ili hiki kipindi kipite salama. Mpenzi msomaji wangu, mada kuhusiana na wapenzi kupeana vijizawadi nadhani ni muhimu kuipata nafasi katika ukurasa huu.
Ni jambo muhimu ambalo mimi na wewe ambao tuko kwenye uhusiano tunatakiwa kulifanya ili kulitia mbolea penzi. Wapo ambao wana katabia ka kuwanunulia wapenzi wao vijizawadi pale wanapowakosea.
Kwa mfano si jambo la ajabu kumkuta mwanaume akiwa amemkera mpenzi wake kumnunulia nguo, simu au kitu kingine na kumpelekea huku akiambatanisha na neno ‘nisamehe’. Hayo yamekuwa yakifanyika huko mtaani na si ajabu hata wewe unayesoma hapa ulishawahi kufanya hivyo.
Lakini pia ishu ya zawadi kwa wapenzi hasa siku za ‘birthdays’ imekuwa ikitiliwa maanani na watu wanaojali. Wale wanaojua maana ya mapenzi! Nasema wanaojua maana ya mapenzi kwa kuwa, wapo ambao hawajawahi hata siku moja kuwanunulia zawadi wenza wao.
Unaweza kukuta wao kila mara wanapewa vijizawadi na kujisikia poa sana lakini kufanya hivyo imekuwa ni ngumu sana kwao. Ninapolizungumzia hili la ugumu wa baadhi ya watu kuwanunulia wapenzi wao zawadi nawagusa wanaume na wanawake. Wapo wanawake ambao wao wamejiweka kuwa ni wa kupokea tu zawadi.
Mbaya zaidi wapo wanaofikia hatua ya kupunguza mapenzi kisa hawapewi vijizawadi. Yaani anataka ikifika ‘bethidei’ yake anunuliwe kitu bila kujali mwenza wake yuko katika hali gani kifedha.
Lakini ukiwaacha hao wanawake, wapo wanaume pia ambao wamekaa kwa kupokea tu. Mifano ya wanaume hao ipo mingi tu huko mtaani. Unamkuta mvulana tangu amekuwa kwenye uhusiano ni wa kununuliwa mara viatu, mara nguo za ndani, mara jinzi kali lakini yeye hata siku moja hutamuona akitoa pesa na kumnunua hata leso kwa ajili ya mpenzi wake. Hii sasa tuite nini?
Ninachojua mimi ni kwamba, mapenzi ni kutoa na kupokea. Vile unavyosikia raha kupokea zawadi kutoka kwa mpenzi wako ndivyo na yeye atakavyofurahi kuona siku moja isiyokuwa na jina umempa zawadi nzuri.
Kama ulikuwa hujui ni kwamba, unapompa zawadi mpenzi wako unaongeza mapenzi lakini pia unapokuwa ni mtu wa kupokea tu, unamfanya mwenza wako akufikirie tofauti. Atajiuliza  kwamba ni kweli huna uwezo wa kumnunulia zawadi hata ndogo?
Je, wewe unamchukuliaje anapokuwa kimbelembele katika kukununulia zawadi? Kwamba yeye anakupenda sana lakini wewe unampenda kidogo? Tusifikie hatua ya kufikiriana hivyo!
Tujenge tabia ya kuwapa zawadi wapenzi wetu tukiwa na dhamira moja tu ya kuonesha upendo wetu lakini pia kumwagilia na kuwekea mbolea penzi letu. Haijalishi unampa zawadi gani!

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top