Featured

Loading...


VIDEO: Wema Sepetu Amrekodi Nuh Mziwanda AKIMTONGOZA........Shilole Azimia Baada ya Video Kusambaa Mtandaoni


Katika hali ya kushangaza, sauti ya mpenzi wa staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ inayosikika akimtongoza Wema Sepetu imemfikia Shilole na kusababisha azimie.

Tukio hilo lililozua mtafaruku lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kulipokuwa na pati ya bethidei ya mwigizaji Shamsa Ford.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kilishuhudia tukio hilo mwanzo-mwisho, saa chache baada ya kumalizika kwa shughuli ya kulishana keki, waalikwa walishangaa kumuona Shilole akiishiwa nguvu na kudondoka baada ya kusikiliza ujumbe wa sauti aliotumiwa kwenye simu.
  
“We acha tu. Ilikuwa balaa. Watu tulikuwa katika shamrashamra ya kulishana keki, ghafla tukashangaa mwenzetu anaishiwa nguvu na kuanguka,” kilieleza chanzo.

Chanzo hicho kilitiririka kuwa, ujumbe huo wa sauti ulisikika Nuh akimuimbisha Wema kwa maneno ya kimahaba.
 
“Nuh kajipambanua ileile. Kaimbisha mistari yote ya kimahaba, utafikiri alikaririshwa. Alijitahidi kushusha vesi tamu ili  kumuingiza Wema kwenye himaya yake. Huwezi amini jamaa alizidisha mbwembwe kiasi cha kumwambia amkubalie kwani hamtaki Shilole tena.

“Wema amesikika akikataa, akamwambia hawezi kuwa naye kwani ni shemeji yake na anamheshimu Shishi,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, baada ya kuusikiliza ujumbe huo, Shilole alimfuata Nuh kwa ajili ya kumsikilizisha lakini Nuh alijibu ‘mbovu’ ndipo Shilole alipomuomba ufunguo wa gari waliyokwenda nayo, akarudi alipokuwa amekaa awali.

“Aliporudi alipokuwa amekaa, Shilole alijikuta akiishiwa nguvu na kuzimia ambapo Aunt Ezekiel na kina JB (Jacob Stephen) walipofanya kazi ya ziada kumpepea, huku wengine wakihangaika kummwagia maji kunusuru afya yake.
 
“Walifanikiwa kumpandisha kwenye gari lake. Joto lilikuwa kubwa kufuatia hali hiyo maana kila mtu alishindwa kuelewa kilichotokea, hivyo Shilole, baada ya kuzinduka aliulizwa kilichomfanya azime ambapo aliwasikilizisha sauti hiyo kila mmoja akabaki ameduwaa,” kilieleza chanzo.

Ilielezwa kuwa, mwigizaji Aunt Ezekiel ndiye aliyeokoa jahazi kwa kulazimika kuendesha gari la Shilole na kumpeleka nyumbani huku Nuh akipandishwa kwenye gari la JB kumpeleka kwa ndugu zake.

Mwandishi wetu, baada ya kupenyezewa habari hiyo, alimtafuta Shilole ili kupata habari kamili ambapo alikiri kupokea ujumbe huo wa sauti huku akiainisha kuwa umemkera kwani kuna maneno yanasikika akimponda yeye.
 
“Inaniuma sana, Nuh kuendelea kunidhalilisha kiasi hicho wakati ni mwanaume ambaye ninamheshimu, tunakoelekea uzalendo utanishinda.

“Nilipousikiliza ujumbe ule kwa mara ya kwanza sikuamini nilichokisikia. Pamoja na Wema kuonesha wazi msimamo wa kumkataa Nuh ila mimi naona kama fedheha kubwa kwangu kwani ninamheshimu sana.
 
“Watu wananiona mimi mkorofi lakini kama ningekuwa napenda kuweka kila jambo wazi, hakuna mtu angeendelea kunifikiria vibaya.
  
“Siwezi tena kuendelea kuumiza moyo wangu kila kukicha,” alisema Shilole ambaye anatumikia kifungo cha Basata kwa kutojishughulisha na sanaa kwa takriban mwaka mmoja kwa kosa la kucheza nusu utupu jukwaani.

Tazama  video  hapo  chini

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top