Tunaendelea kuchambua njia mbalimbali za kuzuia mwanamke kushika mimba, leo tunaanza na kusimulia njia ya kitanzi:
Kitanzi (au koili) kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98 na 99. Na pindi kikitolewa asili ya uwezo wa mwanamke wa kushika mimba anapofanya ngono, unarudi vilevile.
Hata hivyo, moja ya matatizo ya kitanzi ni kwamba vinaweza kuifanya hedhi yako kuwa nzito (damu kutoka nyingi) na pia huenda ukapatwa na maumivu, mara nyingine inaweza kutoka mahali kilipowekwa kikasukumwa nje ya mfuko wa uzazi.
Hivyo ni vyema kumuona daktari mara kwa mara ili kama kimechomoka, kipachikwe tena vyema.
Vasectomy au Tubuligation - Hii ndiyo njia pekee ya kudumu ya kuzuia mimba.
Vasectomy au Tubuligation - Hii ndiyo njia pekee ya kudumu ya kuzuia mimba.
Vasectomy ni njia ya kumfanya mwanaume asiwe na uwezo wa kutunga mimba ilhali Tubuligation ni njia ya kumfanya mwanamke asiwe na uwezo wa kushika mimba. Hii inafanyika kwa njia ya upasuaji mdogo.
Mwanaume anafanyiwa upasuaji kwa kukata vibomba vinavyopitisha mbegu za kiume kutoka kwenye korodani hadi kwenye uume. Upasuaji huu kwa mwanamke unahusisha kukatwa au kuzibwa kwa vibomba vinavyopitisha mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi.
Baada ya upasuaji huu, ni vigumu mwanamke au mwanaume kurudishwa tena katika hali ya mwanzo ya kuweza kuzaa, kwa hivyo njia hii inatumiwa tu kwa sababu za kimatibabu au ikiwa mhusika amefikia uamuzi wa hakika kwamba hataki tena kupata watoto.
Kitanzi cha Intra uterine system au IUS - Hiki nacho kimetengezwa kwa plastiki, yenye muundo wa T kikiwa na chechembe za homoni ya Progestogen ndani. Kinaweza kupachikwa ndani ya mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.
Kitakapopachikwa, Progestogen pole pole huingia ndani ya mwili na kuzuia mimba katika njia ileile kama zinavyozuia tembe. Kinaweza kutumika kwa muda wa miaka 5 na kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 99.
Post a Comment