Featured

Loading...


Waasi wa Burundi Wapanga Kumpindua Rais Nkurunziza


Mmoja wa viongozi wa mapinduzi yaliyozimwa nchini Burundi hivi karibuni ya kutaka kumwondosha madarakani Rais Pierre Nkurunziza, amesema mikakati mingine inaendelea kupangwa ili kumng’oa kiongozi huyo madarakani. 
 
Waasi hao wameyaambia mashirika ya habari ya kimataifa kuwa wamekuwa wakiwapa mafunzo polisi na askari kwa ajili ya jaribio lingine la kumwondoa Rais Nkurunziza.
 
Wamesisitiza kuwa azma ya kumwondosha kiongozi huyo madarakani bado ipo palepale na kwamba kinachoendelea kufanyika sasa ni kuratibu mikakati ya kufanikisha mpango huo.
  
 “ Wakati ule (Mei) tulishindwa kumwondosha Rais Nkurunziza madarakani”, alisema Jenerali Leonard Ngendakumana wakati akihojiwa na shirika la habari la Reuters na kuongeza kuwa; “ mkakati wetu bado uko palepale,”.
 
Wapinzani hao wanampinga hatua ya Rais Nkurunziza kuwania muhula mwingine wa tatu wa uongozi kwa maelezo kuwa kitendo hicho kinakiuka katiba na kwenda kinyume na maridhiano ya Arusha yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Katika hatua nyingine kuna ripoti kuwa, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ameashiria uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika baadaye mwezi huu.
 
Shirika la Habari la China,Xinhua limemnukuu Rais Nkurunziza akitangaza hayo katika moja ya kampeni zake za uchaguzi huo.
 
Rais huyo amesikika akisema kuwa hatua hiyo inakwenda sambamba na mapendekezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyotaka kuahirishwa uchaguzi huo ili kupisha upatanishi.
 
Uchaguzi wa Rais nchini Burundi umepangwa kufanyika Julai 15 lakini Jumuiya ya Afrika Mashariki imependekeza kusogezwa mbele kwa uchaguzi huo ili kumpa nafasi mpatanishi wa jumuiya hiyo, Rais Yoweri Museveni wa Uganda ya kuweza kuzungumza na kuzipatanisha pande zinazoendelea kuhasimiana.
 
Tangu Aprili 26 mwaka huu, Burundi imetumbukia kwenye mgogoro wa kisiasa baada ya Rais Nkurunziza kutangaza nia ya kugombea urais kwa kipindi cha tatu mfululizo.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top