OMARY Faraji Nyembo, anayefahamika zaidi kimuziki kama Ommy Dimpoz ni msanii mwenye jina kubwa katika fani, ingawa ni miongoni mwa vijana waliochipukia na kupata umaarufu katika miaka ya hivi karibuni.
Amefanya kazi nyingi nzuri na zilizopata kupigwa sana katika vituo vingi vya redio na televisheni, baadhi yake vikiwa ni pamoja na Baadae, Me and You, Ndagushima na Wanjera, kitu kinachomfanya kuwa miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri katika soko la Bongo Fleva kwa sasa.
Ingawa hatambi sana, lakini uwezo na kazi zake kwa sasa unamfanya kuwa mmoja wa wasanii ambao kukosekana kwake katika shughuli yoyote kubwa ya burudani ni kero kwa mashabiki. Anategemewa kuwepo miongoni mwa vijana kumi bora wa muziki wa kizazi kipya.
Kwa upande wake, Martin Kadinda ni miongoni mwa wabunifu vijana wa mavazi hapa nchini, ingawa fani hii haimpi jina sana kama ile ya kuwa meneja wa muigizaji Wema Sepetu. Lakini kiukweli, Martin yupo sana kwenye ubunifu na mitindo.
Nimemfahamu kitambo kidogo, akishiriki kupanda jukwaani kusindikiza nguo zilizobuniwa naye au ‘dada zake’ Khadija Mwanamboka na Asia Idarous au wabunifu wenzake akina Ally Rhemtulah.
Nimemfahamu kitambo kidogo, akishiriki kupanda jukwaani kusindikiza nguo zilizobuniwa naye au ‘dada zake’ Khadija Mwanamboka na Asia Idarous au wabunifu wenzake akina Ally Rhemtulah.
Ingawa amekuwa katika ubunifu kwa muda mrefu, nikiri kwamba hakuweza kupata jina alilostahili. Ajabu kwamba amefahamika sana kwa kuwa Meneja wa Wema! Lakini katika hali ya kusikitisha sana, wiki iliyopita katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kwa nyakati tofauti, vijana hawa ‘mabitozi’, waliweka picha kwenye akaunti zao, wakionesha maumbile yao makubwa ya kiume.
Bila shaka, lengo lao lilikuwa ni kuwaonesha marafiki zao jinsi gani ‘walivyojaaliwa’ kwani upo msemo mitaani kuwa wanawake wengi hupenda wanaume wenye maumbile makubwa. Huenda wengi waliamini hivyo, imani ambayo ilikuja kuyeyuka, baada ya muigizaji wa filamu Salma Jabu ‘Nisha’ naye kuposti picha, akionekana kuwa na maumbile ya kiume.
Ndipo ikafahamika kuwa vijana wale wa kiume, waliweka kiungo feki cha uzazi. Sijajua ni kwa lengo gani waliweka. Yapo maneno mitaani ambayo hayawasemi vizuri vijana hawa, ingawa nisingependa kulizungumzia kwa vile ninakosa ushahidi.
Lakini kwa namna yoyote, kwa jina na hadhi zao, ni ukosefu wa maadili kuweka picha kama hizo sehemu ambayo kila mtu ataiona. Unapiga picha maumbile yako, unaweka hadharani, kwa sababu zipi?
Lakini kwa namna yoyote, kwa jina na hadhi zao, ni ukosefu wa maadili kuweka picha kama hizo sehemu ambayo kila mtu ataiona. Unapiga picha maumbile yako, unaweka hadharani, kwa sababu zipi?
Ninajua kuna akina dada wanaojipiga picha za nusu utupu, zinazoonesha sehemu kubwa ya maungo yao na baadaye picha hizo wanaziweka katika mitandao ya kijamii. Lakini si hivyo tu, wengine hupiga picha za kawaida zenye kuwaonesha walivyo na kuziweka kwa lengo la kuwavutia wanaume.
Hawa tunawajua na biashara zao zinajulikana. Sasa vijana kama Ommy Dimpoz na Martin Kadinda, picha zile ni kwa ajili ya kunadi biashara gani inayotokana na viungo mlivyoweka?
Nadhani kuna ulimbukeni flani miongoni mwa masupastaa wetu, ambao wanashindwa kutumia majina na umaarufu wao kukamata fursa za kuwasaidia kubadili maisha yao. Ni mtangazaji gani atavutiwa na mtu anayepiga picha zilizokosa heshima kama hizo ili afanye naye tangazo la kupromoti kampuni au bidhaa yake?
Na ujinga kama huu hauko tu kwa Dimpoz na Kadinda, bali kwa vijana wengi waliotumia nguvu kubwa kupata umaarufu katika muziki, filamu au sanaa nyingine. Ukubwa wa jina la mtu ni mtaji kibiashara.
Watangazaji wengi wanapenda kufanya kazi na mastaa wasiokuwa na skendo au wasiofanya mambo ya aibu hadharani, kwani upo uwezekano wa washindani wao kutumia upungufu huo kuwamaliza.
Post a Comment