1. Ana mahusiano mazuri na baba yake (kama baba yake bado yupo), halafu kama mshua wake ni mume bora kwa mama yake basi ukikuta una boyfriend anamkubali dingi wa aina hiyo na kujifunza mambo kutoka kwake then be sure kwamba that dude will be a good husband kwako.
2. Hafuati mifano mibaya. Yani kama boyfriend wako ana dingi mizinguo, asiyejali familia, etc basi kama yeye hafuati mifano ya huyo buda wake na anamchana live kwamba mzee unachofanya sio sawa then you can be sure this guy will be a good husband.
3. Yuko karibu na wadogo zake wa kiume, mabinamu, sisters, etc. Mwanaume ambaye yuko karibu na ndugu zake wadogo hasa ku act kama mshauri wao, etc ni dalili atakuwa baba na mume mzuri. Mfano ukiona una boyfriend ambaye ndugu zake wadogo daily wanamcheki kumuomba ushauri then that’s a good sign. Mshikilie, he will be a good husband and dad. Mfano unakuta home kwao hawako poa ila jamaa anasaidia hapa na pale like kulipa ada za madogo zake, etc. Ila ukiona he doesn’t care about ndugu zake anza kuwa na wasiwasi.
4. Ana msimamo, hayumbishwi na pressure na ya ajabu ajabu. A.k.a ana mustendi. Sio mtu wa kuyumba yumba kwenye maamuzi.
5. Marafiki zake ni watu wazuri. Ukiona mpenzi wako ana marafiki wa ajabu ajabu basi pata mashaka sana.
6. Anaheshimu wanawake wote. Kuanzia mama yake mzazi hadi muhudumu wa baa.
7. Anapenda watoto hata kama sio wake au wa karibu na yeye. Sio akiona watoto anakunja uso.
8. Anajiheshimu. Sio mtu wa hovyo hovyo.
9. Anazungumzia kuhusu mipango ya ndoa. Sio una-date mtu 5 years hata siku moja hajawahi kugusia kuhusu kuoana.
Post a Comment