Featured

Loading...


Mwandosya Arejesha Fomu za Urais


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya amerejesha fomu zake za kuwania kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais.
 
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha fomu yake alisema akichaguliwa kuwa rais atahakikisha kuwa na utawala bora, kuboresha huduma za jamii na kuhakikisha amani na usalama wa nchi unadumishwa.
 
Profesa Mwandosya ambaye amekuwa mgombea wa 12 kurejesha fomu ambayo ilipokelewa na katibu wa oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib, alisema pia kwamba amefurahishwa na wagombea wenzake ambao amesema kwamba watamuunga mkono.
 
Mpaka juzi wanachama 40 wa CCM amechukua fomu kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba.
 
Tarehe ya mwisho ya urejeshaji wa fomu ni Julai 2. Profesa Mwandosya amesema kwamba amefurahishwa sana na kauli za wagombea wenzake kwamba watamuunga mkono kama atapitishwa na CCM kuwa mgombea.
 
Aidha amesema kwamba anamshauri mgombea mwenzake wa nafasi hiyo, waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kufanya kama hao wengine ili kurahisisha kazi ya CCM kupata mgombea wake katika nafasi ya Urais.
 
Alisema kwamba ametembea katika mikoa 31 katika harakati za kutafuta wadhamini na kuwapongeza viongozi wa chama chake katika wilaya kwa kufanikisha uratibu uliowezesha wagombea kupata wadhamini.
 
“Hata hivyo nimewasilisha udhamini kutoka mikoa 12 ya Bara na mitatu ya Zanzibar zikiwa na wadhamini 30 kwa kila mkoa na kufanya jumla ya wadhamini kuwa 450 wanaotakiwa na chama,” alisema Profesa Mwandosya.
 
Aliitaja mikoa hiyo kuwa Dodoma, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Mjini Unguja, Unguja Kusini, Unguja Magharibi, Pemba Kusini, Pemba Kasikazini, Tanga, Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga, Simiyu, Mara, Songea, Njombe, Iringa, Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top