Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ubora wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala wa baraza hilo Twilumba Mponzi na Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex Nkondola.
Wakurugenzi wa Manejimenti ya NACTE wakiwa kwenye mkutano pamoja na waandishi wa habari uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha EAT, Noah Laltaila akimuuliza swali Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga kwenye mkutano uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Baadhi ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE) uliohusu kutangaza ubora wa elimu unaotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
HOTUBA YA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) DKT ADOLF B. RUTAYUGA KUHUSU TAMKO LA BARAZA LA KUVIFUTIA USAJILI BAADHI YA VYUO NA KUVISHUSHA HADHI VINGINE – 24/06/2015
Ndugu waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, ninayo furaha kubwa kuwakaribisha katika ofisi za Baraza. Lengo la kuwaita hapa leo ni kuwapa taarifa juu ya maamuzi yaliyofikiwa na Baraza ikiwa ni katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini.
Ndugu Waandishi wa Habari
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Kwa kutumia Sheria na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujirekebisha.
Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi kama vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali Na. 1, Jedwali Na. 3, na baadhi kwenye Jedwali Na. 5 vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Hata hivyo, hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4.
Tamko la Baraza
Kutokana na mapungufu hayo Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4 kwa makosa yafuatayo:
- a) Ama kumalizika kwa muda wa Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); au
- b) Kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; au
- c) Kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukua hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na
- d) Taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali.
Jedwali Na. 1: Taasisi na Vyuo vinavyoruhusiwa kuendelea na taratibu za Usajili baada ya kutimiza masharti
Na
| Jina la Chuo/Taasisi | Namba ya Usajili |
1 | Regional Aviation College – Dar es Salaam | REG/EOS/028P |
2 | Zoom Polytechnic College – Dar es Salaam | REG/EOS/030P |
3 | Gataraye Research and Training Centre – Dar es Salaam | REG/EOS/034P |
4 | Modern Commercial Institute (MCI) – Dar es Salaam | REG/BMG/024P |
5 | Evin School of Management – Dar es Salaam | REG/BMG/026P |
6 | Agape School of Management – Dar es Salaam | REG/BMG/027P |
Jedwali Na. 2: Taasisi na Vyuo vilivyofutiwa Usajili na kuzuiliwa kudahili wanafunzi wapya baada ya kutotimiza masharti ya Usajili
Na. | Jina la Chuo/Taasisi | Namba ya Usajili/Maelezo |
1 | Dar es Salaam College of Clinical Medicine – Kinondoni | Usajili wa Awali |
2 | Ndatele School of Medical Laboratory Sciences – Dar-es-Salaam | Usajili wa Awali |
3 | Institute for Information Technology – Dar es Salaam | REG/EOS/014 |
4 | DARMIKI College of Educational Studies | Hakijasajiliwa. Kimezuiliwa kudahili wanafunzi |
Jedwali Na. 3: Taasisi na Vyuo vinavyoruhusiwa kuendelea na taratibu za Ithibati baada ya kutimiza masharti
Na. | Jina la Taasisi/Chuo | Namba yaUsajili | Hadhi Kabla yaNotisi | Hadhi Baada yaNotisi |
1 | Mabughai Community Development Technical Training Institute – Lushoto | REG/EOS/040 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
2 | Kizimbani Agricultural Training Institute – Zanzibar | REG/ANE/027 | Usajili Kamili | Ithibati ya Awali |
3 | Civil Aviation Training Centre – Dar es Salaam | REG/EOS/006 | Ithibati ya Muda | Ithibati ya Muda |
4 | Ardhi Institute – Tabora | REG/EOS/010 | Ithibati ya Muda | Ithibati Kamili |
5 | Bandari College – Dar es Salaam | REG/EOS/018 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
6 | Tanzania Institute of Rail Technology – Tabora | REG/EOS/012 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
7 | RETCO Business College (RBC) – Iringa | REG/BMG/025 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
8 | Aseki Business School – Dodoma | REG/BMG/030 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
9 | Western Tanganyika College – Kigoma | REG/BMG/032 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
10 | Law School of Tanzania | REG/BMG/040 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
11 | Royal College of Tanzania (RCT) – Dar es Salaam | REG/PWF/004 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
12 | Tanzania Regional Immigration Training Academy (TRITA) – Moshi | REG/PWF/030 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
13 | Morogoro School of Journalism (MSJ) – Morogoro | REG/PWF/005 | Ithibati ya Muda | Ithibati ya Muda |
14 | Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) – Bagamoyo (former Bagamoyo College of Arts – Bagamoyo) | REG/PWF/010 | Ithibati Kamili | Ithibati Kamili |
15 | Newman Institute of Social Work (NISW) – Kigoma | REG/PWF/016 | Ithibati Kamili | Ithibati Kamili |
16 | Njuweni Institute of Hotel, Catering & Tourism Management – Kibaha | REG/ANE/016 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
17 | Geita School of Nursing – Geita | REG/HAS/079 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
18 | St. Gaspar Nursing School – Itigi | REG/HAS/090 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
19 | Bugando School of Nursing – Mwanza | REG/HAS/052 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
20 | COTC Mafinga – Iringa | REG/HAS/047 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
21 | Kagemu School of Environmental Health Sciences – Bukoba | REG/HAS/034 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
22 | Mvumi Institute of Health Sciences – Dodoma | REG/HAS/011 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
23 | Tanzania Training Centre for International Health – Ifakara | REG/HAS/003 | Ithibati ya Muda | Ithibati ya Muda |
24 | Mbeya Polytechnic College (former Ilemi Polytechnic College) – Mbeya | REG/BMG/031 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
25 | Institute of Sports Development Malya – Mwanza | REG/PWF/019 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
26 | Ruaha Community Development Training Institute (CDTI) – Iringa | REG/PWF/028 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
27 | Uyole Community Development Training Institute (CDTI) – Mbeya | REG/PWF/027 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
28 | Institute of Rural Development Planning (IRDP) – Mwanza | REG/PWF/043 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
29 | Rungemba Community Development Institute (CDTI) – Mufindi | REG/PWF/007 | Ithibati Kamili | Ithibati Kamili |
30 | Time School of Journalism (TSJ) – Dar es Salaam | REG/PWF/013 | Ithibati Kamili | Ithibati Kamili |
31 | COTC Machame – Hai | REG/HAS/087 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
32 | Mwambani School of Nursing – Chunya | REG/HAS/089 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
33 | Kiomboi School of Nursing – Iramba | REG/HAS/091 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
34 | College of Health Sciences Zanzibar | REG/HAS/095 | Usajili Kamili | Usajili Kamili |
35 | Kabanga School of Nursing – Kasulu | REG/HAS/023 | Usajili Kamili | Ithibati ya Awali |
36 | Kondoa School of Nursing – Dodoma | REG/HAS/040 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
37 | Lugarawa School of Nursing – Ludewa | REG/HAS/036 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
38 | Tosamaganga School of Nursing – Iringa | REG/HAS/020 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
39 | Vector Control training Centre – Muheza | REG/HAS/031 | Ithibati ya Muda | Ithibati ya Muda |
40 | Training Centre for Health Records Technology – Moshi | REG/HAS/072 | Ithibati ya Muda | Ithibati ya Muda |
41 | Dar es Salaam School of Journalism (DSJ) – Dar es Salaam | REG/PWF/012 | Ithibati Kamili | Ithibati Kamili |
42 | Financial Training Centre – Dar es Salaam | REG/BMG/004 | Ithibati ya Awali | Ithibati ya Awali |
Jedwali Na. 4: Taasisi na Vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kutotimiza masharti ya Ithibati
Na. | Jina la Taasisi/Chuo | Namba yaUsajili | Hadhi Kabla yaNotisi | Hadhi Baada yaNotisi |
1 | Sura Technologies – Dar es Salaam | REG/EOS/019 | Usajili Kamili | Usajili wa Muda |
2 | Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam | REG/EOS/016 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
3 | Techno Brain – Dar es Salaam | REG/EOS/021 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
4 | Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya | REG/ANE/009 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
5 | Mbozi School of Nursing – Mbeya | REG/HAS/062 | Usajili Kamili | Usajili wa Muda |
6 | KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi | REG/HAS/085 | Usajili Kamili | Usajili wa Muda |
7 | KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi | REG/HAS/094 | Usajili Kamili | Usajili wa Muda |
8 | Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi | REG/HAS/076 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
9 | AMO Training Centre Tanga – Tanga | REG/HAS/049 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
10 | CATC – Songea | REG/HAS/054 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
11 | CATC – Sumbawanga | REG/HAS/055 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
12 | COTC Maswa – Shinyanga | REG/HAS/014 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
13 | COTC – Musoma | REG/HAS/033 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
14 | Dental Therapists Training Centre – Tanga | REG/HAS/057 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
15 | Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba | REG/HAS/058 | Ithibati ya Awali | Usajili wa Muda |
16 | KCMC AMO General School – Moshi | REG/HAS/096 | Ithibati ya Muda | Usajili Kamili |
Jedwali Na. 5: Taarifa kuhusu Taasisi na Vyuo vyenye maelezo maalum
Na. | Jina la Taasisi/Chuo | Namba yaUsajili | Hadhi Kabla yaNotisi | Hadhi Baada yaNotisi | Maelezo |
1 | Lake Teachers College – Singida | REG/TLF/001 | Usajili wa Muda | Usajili Kamili | Kimeruhusiwa kudahili wanafunzi |
2 | Patricia Metzger Academy of Health and Beauty – Dar-es-Salaam | REG/PWF/022P | Usajili wa Muda | Usajili wa Muda | Kimesitisha kutoa mafunzo |
3 | Institute of Management and Entrepreneurship Development – Dar es Salaam | REG/BMG/039 | Usajili Kamili | Usajili Kamili | Kimesitisha kutoa mafunzo |
4 | Tanga School of Nursing – Tanga | REG/HAS/084 | Ithibati Kamili | Ithibati Kamili | Haijamaliza muda wa Ithibati |
5 | ESACS School of Journalism and Business Studies – Dar es Salaam | REG/PWF/044 | Usajili Kamili | Usajili Kamili | Kimesitisha kutoa mafunzo |
6 | Fire and Rescue Training Centre – Dar es Salaam. | REG/EOS/032P | Usajili wa Muda | Usajili wa Muda | Kimesitisha kutoa kozi za muda mrefu. Sasa kinatoa kozi za muda mfupi ambazo hazipitishwi na Baraza (NACTE). |
Asanteni kwa kunisikiliza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
24 JUNI 2015
Post a Comment