Staa wa bongo fleva ambaye ameshawahi kucheza filamu kadhaa za hapa Bongo, kwa sasa ameanza kujikita katika siasa za nchi Keisha amefunguka na kuwahamasisha vijana kujitambua pamoja na kuwataka kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuwa na tija katika maisha yao kwa kuwataka kutojidharau wenyewe kwani wakijidharau hali hiyo itapelekea wao wenyewe kukata tamaa ya maisha na kushindwa kufanya mambo ya kimaendeleo. Keisha ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
"Uthubutu ni ile hali ya kuwa na msukumo/shauku ndani ya moyo wa kujaribu jambo fulani.Mara nyingi watu wanakosa uthubutu kutokana na kutojiamini kuwa yeye vile alivyo anaweza kufanya mambo makubwa na ya ajabu bila kujali kiwango cha elimu,
pesa, mtandao aliyo nayo. Watu hutazama madhaifu yao wenyewe na mazingira yanayowazunguka mwisho hukata tamaa na kusema mm siwezi.Matajiri wote duniani baada ya kuwa na mawazo walithubutu licha ya ugumu na changamoto walizopitia leo hii kwao imebaki historia wanakula kuku kwa mrija. Acha kujidharau, Mungu ametuumba kuwa washindi, na amekuleta duniani kwa makusudi kabisa sio kwa bahati mbaya.Kuna watu wapo nyuma yako wanasubiri uthubutu ukifanyikiwa wewe uwe mfano wao." Alisema Keisha

Lakini msanii huyo hakuishia hapo alizidi kutoa hamasa kwa vijana mbalimbali nchini kujaribu katika nyanja mbalimbali na kusema kufanya uthubutu ni jambo ambalo linaweza kubadili dila yao ya maisha na kuwa na mafanikio kama watu wengine, hivyo awataka wajaribu katika michezo, mpira, muziki, filamu kwani kupitia sanaa ndiyo sehemu pekee ambayo inaweza kuleta mabadiliko ya haraka ikiwa ukiweza kukufanyia kazi kwa makini.
"Thubutu leo iwe kwenye elimu, biashara, siasa, michezo, mziki, filamu na mafanikio utayaona.Jikubali kwanza unaweza kwani uthubutu wako ndiyo tiketi yako katika mafanikio yako". Alimalizia Keisha
EATV.TV
Post a Comment