Baadhi ya Wanalyalamo Family katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Winfrida Lubanza (wa tatu kulia).
Na mwandishi wetu
WITO umetolewa kwa Watanzania nchini kujitolea kwa hali na mali kusaidia watu wenye uhitaji ikiwemo watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali.
Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund kilichopo Chanika, jijini Dar es Salam, Winfrida Lubanza wakati akizungumza na wanafamilia wa Lyalamo.
Alisema jamii inapaswa kuwakumbuka na watoto waliopo katika vituo hivyo kwani wanastahili kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu kama ilivyo kwa watoto waliopo majumbani.
"Watoto yatima ni watoto kama wengine nao wana uhitaji sawa hivyo jamii isiwasahau na kwani nao wanapata furaja na kupata matumaini zaidi,"alisema

Aidha, aliongeza kuwa kituo chake kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo chakula, madawa, sabuni na ada kwa wanafunzi sambamba na mtaji wa kuwezesha kuanzisha biashara ambayo itaweza kuwapatia pesa za kujikimu.
"Tunachangamoto nyingi mfano kuna mwanafunzi yupo kidato cha nne amerudishwa kituoni sababu hatujakamilisha ada,"alisema
Naye kiongozi wa Lyalamo Family, Aziza Kibwana alisema wamefarijika kufika kituoni hapo na kuona changamoto hizo hivyo watajitahidi kuchangia walichojaaliwa.Pia amesisitiza wadau kujitokeza kusaidia.
"Sisi tumesoma shule za msingi za bweni tukiwa wadogo na tulikuwa na watoto kutoka katika vituo kama hivi hivyo tunaguswa sana na hali zao ndio maana tuko hapa," alisema
Aziza aliongeza kwamba kupitia umoja wao watajitahidi kadiri wawezavyo kuvifikia vituo mbalimbali na kutoa misaada.
"Humu kuna marais, kuna mawaziri, wabunge, wanasoka, wasanii, wafanyabiashara, madaktari, wahasibu n.k sasa ni muhimu kuwakumbuka na watoto waliopo huku ili kuwajengea misingi mizuri ya kutimiza ndoto zao," aliongeza
Katika ziara yao, Lyalamo Family walikabidhi kituoni hapo vyakula, mafuta, dawa, madaftari, sabuni na vitu vinginevyo ambapo watoto waliopo kituoni hapo walifurahi na kushukuru.
Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2001 kinalea watoto kati ya 150 hadi 300 wenye umri chini ya miaka 18.

Post a Comment