Featured

Loading...


KEMIKALI ZINAVYOATHIRI SEHEMU ZA SIRI ZA WANAWAKE

Wanawake hupenda sana kutumia marashi na vitu vingine kama sabuni zenye kemikali kwa ajili ya kujirembesha.
Baadhi yao wamekuwa wakipenda usafi wao binafsi wakitumia vitu  ambavyo baadhi yake ni hatari kwani wengine wanapenda kusafisha sehemu zao za siri kwa kutumia sabuni zenye kemikali, pafyumu yaani ‘deodorant’ au kupaka mafuta bila kujua madhara yake.
Wanawake hao wanaotumia vitu hivyo wana hatari ya kupata magonjwa ya zinaa au ya kuambukiza. Watafiti katika Chuo Kikuu cha California, Marekani wanasema sabuni ngumu au hata za maji, pafyumu ‘deodorant’ zinaharibu tishu muhimu zilizomo ndani kabisa ya uke.
Uharibifu huo wa tishu ndani ya sehemu za siri humweka mhusika katika hatari ya kupata malengelenge, fangasi  vitu ambavyo huweza kusababisha kupata Ukimwi ikiwa watajamiiana na watu wenye tatizo hilo.
Sabuni au dawa zinazouzwa na wafanyabiashara zikitangaza kuboresha uke au kuondoa harufu kwenye sehemu hizo nyeti nazo zina madhara.
Sabuni au mafuta yenye kemikali  huchubua ngozi laini ya uke na ni rahisi vimelea vya magonjwa kuenea kwa urahisi.
Michubuko hiyo ambayo si rahisi kuonekana kwa macho ndicho chanzo cha kuingia kwa maradhi ya kuambukiza.
Kutokana na hayo ni wazi kwamba hakuna haja ya kuweka kemikali, au pafyumu ukeni. Hizo sehemu zinahitaji kuoshwa vizuri kwa maji safi.
Kemikali inapoingia ukeni inavuruga hali ya kawaida na asidi inayolinda sehemu hizo ni vyema wanawake wakaelimishwa kuhusu matumizi ya bidhaa zinaweka harufu nzuri katika sehemu zao za siri, kurudisha bikira au mafuta ya kulainisha uke.
Wanawake wanaofanya usafi sehemu zao za siri kwa kutumia bidhaa au baadhi ya vifaa visivyofaa kutumiwa ukeni huweza kupata saratani ya shingo ya uzazi.
Bidhaa zenye kemikali ya ‘coal tar,’ ambazo mara nyingine huwekwa kwenye sabuni ama manukato na kutumiwa ukeni na wanawake huweza kuchochea saratani hiyo.
Upo ushahidi wa kutosha kuwa kutumia sabuni za kuogea za maji au ngumu katika sehemu za siri za ndani za mwanamke kunaharibu uwiano wa bakteria na kusababisha bakteria kuzalishwa kwa wingi na kumweka mwanamke katika hatari ya maradhi ya  zinaa ya kuambukiza.
USHAURI
Acha kutumia sabuni zenye kemikali au pafyumu sehemu za siri kwani husababisha hayo niliyoyataja hapo juu.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top