CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.
Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?
Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema, upinzani wa kweli, utatoka CCM. Jee hiki ndio kipindi cha upinzani huu?
Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?
Jee Lowassa tuliombatiza jina la mwamba, ataliishi hilo jina la mwamba kwa kuonyesha umwamba wake kwa kutokubali kuchinjwa na kufanywa mbuzi wa shughuli, au lile jina la mwamba, tulimpachika tuu, ila in reality kumbe sii mwamba lolote wala chochote, bali ni kichuguu tuu?
Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?
Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?
Pasco!
Post a Comment