Simanzi! Mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu na Mwanzilishi wa Kanisa la Cathedral of Joy (CoJ) na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Askofu John Simon Komanya aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa kisukari, yamekuwa gumzo baada ya familia yake kufuatilia maziko kidijitali kwenye mtandao wa kijamii wa Skype wakiwa Marekani.
Mazishi ya askofu huyo yaliyoshuhudiwa na waandishi wetu yalifanyika Jumatano wiki hii kwenye kanisa lake lililopo Gogoni, Kiluvya jijini Dar na kuongozwa na maaskofu, wachungaji, waimbaji wenzake na umati mkubwa wa waombolezaji.
Akizungumza na waandishi wetu, mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Abel Kigeli alisema Askofu Komanya alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu lakini Julai 29, mwaka huu hali yake ilibadilika na kukimbizwa katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar.Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
“Hali yake ilibadilika hivi karibuni na alipopelekwa Hindu Mandal hali ilizidi kuwa mbaya na Julai 4, akahamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na siku hiyohiyo Mungu alimpenda zaidi na kumpumzisha, lakini sisi kanisa tutaendeleza kazi yake kama alivyokuwa akiifanya enzi za uhai wake,” alisema Mchungaji Kigeli.
Waimbaji mbalimbali wa Injili walijumuika kwa pamoja kumzika Askofu Komanya ambapo waligawana majukumu mbalimbali na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa huku mwimbaji, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ akigeuka kivutio muda wa msosi kwa namna alivyokuwa akiwahudumia waombolezaji.
Wachungaji kutoka makanisa mbalimbali jijini Dar walitoa maneno yao kufuatia msiba huo wa mwenzao kuwa kifo chake kimetokana na mapenzi ya shetani lakini kazi aliyotumwa bado haijaisha na wao watahakikisha wanaiendeleza.
Kwa upande wake Akofu Mkuu wa Makanisa ya Calvary, Dunstan Maboya alisema: “Komanya alikuwa muimbaji kama waimbaji wengine lakini mimi nilipokutana naye kwa mara ya kwanza ndiyo nikamshauri akasomee uaskofu kwani waimbaji wengi huishia kuwa wachungaji tu.
Kwa upande wake Akofu Mkuu wa Makanisa ya Calvary, Dunstan Maboya alisema: “Komanya alikuwa muimbaji kama waimbaji wengine lakini mimi nilipokutana naye kwa mara ya kwanza ndiyo nikamshauri akasomee uaskofu kwani waimbaji wengi huishia kuwa wachungaji tu.
Ndugu na familia ya marehemu John Komanya walionesha kuhuzunishwa na kifo cha ndugu yao na kudai kuwa ndiye alikuwa mpiganaji wao, lakini kwa upande wa mke wake na watoto wao walishuhudia mazishi ya baba yao kupitia Skype.
Marehemu Komanya ameacha mke na watoto watatu, wawili wa kike. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen.
Post a Comment