Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka.
Vipande viwili vya fuvu la binadamu.
Chupa tatu za mafuta ya simba alizokutwa nazo mtuhumiwa.

Vipande viwili vya fuvu la binadamu.
Chupa tatu za mafuta ya simba alizokutwa nazo mtuhumiwa.
Vipande vya ngozi ya simba
JESHI la polisi mkoani Singida
linamshikilia mkazi moja wa Kijiji cha Itumba, wilaya ya Igunga, mkoani
Tabora kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu na nyara za
serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka,
amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Magida Bundala aliyekamatwa akitoka mkoani
Tabora kuja Singida kusalimia ndugu zake ambao walikuwa wamewekwa
mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ikungi.
Kamanda Sedoyeka alisema walimkamata
mtuhumiwa huyo baada ya askari kumtilia mashaka na kuamua kumkagua
wakati akisubiri kuwasalimia ndugu zake ambao ni mahabusu alipokutwa na
vipande viwili vya fuvu la binadamu, ngozi ya chatu, vipande vya ngozi
ya simba, pembe ambayo haijajulikana kuwa ni ya mnyama gani na chupa
tatu za mafuta ya simba.
Wakazi wa Manispaa ya Singida wameliomba
jeshi la polisi kuhakikisha linamfuatilia mtuhumiwa huyo ili kubaini
mtandao mzima kwa sababu unaendesha shughuli zao kutokana imani potofu
ikiwa ni pamoja kupata madaraka, jambo ambalo husababisha vifo kwa
binadamu wakiwemo walemavu wa ngozi (albino).
CHANZO: IVT


Post a Comment