UNAZI! Kundi kubwa la vijana wa kike na kiume, mwanzoni mwa wiki iliyopita walizua kizaazaa baada ya kumgombea kumuona kwa karibu na kutaka kuzungumza na mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ mara baada ya kumaliza kutumbuiza katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli uliofanyika katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba.

Umati huo ukigombea kumuona Diamond.
Baada ya kumaliza ngwe yake ya kuburudisha, msanii huyo aliteremka
jukwaani na kwenda alikopangiwa kukaa, lakini alifuatwa na dada mmoja
aliyetaka kuzungumza naye, huku vijana wengine wakisogea eneo hilo, kitu
ambacho mabaunsa walikikataa na kumfanya msanii huyo kukimbilia katika
basi dogo aina ya Coaster lililokuwa limetayarishwa kwa ajili yake na
wacheza shoo wake.Hata hivyo, wakati mkutano huo ukiendelea, umati zaidi wa vijana uliendelea kulifuata basi hilo na kujazana katika dirisha alilokaa Diamond, jambo lililowapa wakati mgumu mabaunsa kuwasogeza, hadi polisi walipofika na kufanikiwa kuwatawanya, huku gari hilo likiondolewa eneo hilo.

Akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni.
Hata hivyo, baada ya basi hilo kupata upenyo wa kumkimbiza
mwanamuziki huyo, kundi kubwa la vijana wa kike na kiume walilifukuza
gari hilo mpaka dereva alipoongeza kasi.Kabla ya mkutano huo mkoani hapa, Magufuli alianza kunadi sera zake katika Vijiji vya Kaziramuyagwa, Kyamyorwa, Kasharunga, Rulanda na kufanya mkutano mkubwa katika Uwanja wa Zimbihile uliopo Muleba Kusini jimbo analogombea Prof. Anna Tibaijuka.
Baada
ya hapo kampeni zilihamia Muleba Kaskazini ambapo Magufuli alimwaga
sera katika maeneo ya viwanja vya wazi vya Kamachumu, Maruku na Jimbo la
Bukoba vijijini kabla ya kufanya mkutano wa kihistoria katika viwanja
vya Bukoba mjini.


Post a Comment