Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli leo akihutibia moja ya mikutano yake ya kampeni aliyoifanya
katika wilaya za Mbogwe, Bukombe mkoani Geita na Kisha Halmashauri pya
ya Ushetu baadaye mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika mjini Kahama
mkoani Shinyanga ambapo mji huo umetikisika kutokana na umati wa
wananchi waliohudhuria mkutano huo uliorushwa moja kwa moja na kituo cha
Televisheni cha Star TV huku baadhi ya wananchi wakisema CCM ilmeleta
Sunami Kahama.
Akizungumza katika mkutano huo
wakati akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu ili
kumpigia kura za ndiyo ili awatumikie watanzania katika nafasi ya Urais
na kuongeza kwamba moja ya mambo ambayo serikali yake itashughulikia ni
pamoja na kuhakikisha madereva wanapata mikataba kutoka kwa waajiri wao
ili kuboresha maslahi yao.
Amesema Madereva ni watu muhimu
sana katika sekta ya usafirishaji na wanafanya kazi ngumu sana lakini
maslahi yao hayajaangaliwa kwa makini na kuyaboresha ili na wao ili na
wao waone faida ya kazi yao, Na siyo kuumia bila kipato
kinachowatosheleza katika kuendesha familia zao na maendeleo yao
kiuchumi. hivyo serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dk. John
Pombe Magufuli italiangalia pia suala hilo.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-KAHAMA)

Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja
wa CCM Kahama.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria
katika mkutano huo wakipunga mikono yao juu kuashiria kufurahishwa na
hotuba ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama
Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli.


Waangalizi wa uchaguzi pia pia walihudhuria katika mkutano huo.

Kutoka kulia ni Mzee Samwel Sitta
Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita
Ndugu Joseph Kasheku Msukuma pamoja na viongozi wengine wa CCM wakiwa
katika mkutano huo.

Mzee Samwel Sitta Mjumbe wa
Kamati ya Ushindi akiwahutubia wananchi wa Kahama katika mkutano wa
kampeni uliofanyika mjini Kahama leo.

Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya
CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi akiwahutubia wananchi katika
mkutano huo uliofanyika mjini Kahama.

Kundi la muziki la Yamoto Bandi
likifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano wa kampeni wa CCM
uliofanyika mjini Kahama na kuhutubiwa na Dk. John Pombe Magufuli.


Msanii Chege kutoka kundi la TMK Wanaume akitumbuiza katika mkutano huo.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli akiwasili katika uwanja wa CCM mjini Kahama kwa ajili ya
kuhutubia mkutano wake wa kampeni huku akipokelewa na picha yake kubwa
iliyochorwa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
CCM Ndugu Abdallah Bulembo akizungumza jambo na mgombea ubunge wa jimbo
la Msalala Mh. Azekiel Maige wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika
mjini Kahama.

Mzee Samwel Sitta Mjumbe wa
kamati ya ushindi ya CCM na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph
Kasheku Msukuma pamoja na viongozi wengine wa CCM wakicheza muziki
katika mkutano huo.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli akizungumza na wananchi ambao ni wachimbaji wadogo na
kuwasalimia wakati akiwa njiani kuelekea Ushetu

Wananchi wa Masumbwe wakimpokea
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha
Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli alipowasili kwenye mji huo na
kufanya mkutano wa kampeni.

Ni kama wanasema Magufuli ni Dole tu.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni katika mji wa
Ushirombo wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Wananchi wa Nyarugusu
wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati akiwahutubia.

Ni shangwe tu kwa kumuona
mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha
Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kahama kupitia CCM Ndugu
Jumanne Kishimba.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli akiwanadi baadhi ya wagombea ubunge wa mkoa wa Shinyanga


Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli na mzee Samwel Sitta wakisakata Rhumba mara baada ya kuhutubia
mkutano huo mjini Kahama.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli akiondoka katika uwanja wa CCM Kahama mara baada ya kuhutubia
mkutano huo




Post a Comment