Wananchi wa Hai Mjini wakimpokea Mwigulu Nchemba kwa shangwe.
Mwigulu
Nchemba ameshawasili Hai Mjini kuzungumza na Wananchi na Kumuombea Kura
Rais Mtarajiwa kutoka Chama cha Mapinduzi Ndg,J.Pombe Magufuli.
Mwigulu
Nchemba akitoa Darasa kwa Wananchi wa Hai Mjini kuhusu Umuhimu wa
Kuchagua kiongozi kwa Malengo,sio kuchagua Uongozi kwa
Kishabiki."Wanahai naomba Mmchague Magufuli kwasababu ndiye kiongozi
anayeweza kushughulika na Matatizo ya Wananchi wetu hasa swala la
Rushwa,Uzembe maofisini na wadhurumaji.Kwa hapa Hai mmeshaonja ubaya wa
Upinzani,hawajishughulishi kwa maendeleo Zaidi ya kupiga kelele
zisizokuwa na tija kwa Wanahai".
Wananchi wa Hai wakisema Nguvu Moja.
Mwigulu Nchemba akiwasili USA river hapo jana.
Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa USA River mapema hapo jana.
Mbunge
mtarajiwa wa Moshi Mjini Ndg.Davis Mosha akisalimiana na Mwigulu
Nchemba wakati wa Mkutano wa hadhara ndani ya kata ya Sokoni.
Mwigulu Nchemba akimnadi Davis Mosha mbunge Mtarajiwa kwa Moshi mjini.
Mwigulu Nchemba akiwasili Same Mashariki.
Mwigulu
Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Same Mashariki Bi.Anna Kilango
Malecela mapema hii leo wakati alipokwenda kuinadi Ilani ya CCM.
Comrade
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Same Mashariki kuhusu
Umuhimu wa kufanya Uchaguzi kwa Amani,Pia kuichagua CCM kwasababu
imefanya kazi kubwa kuiletea Maendeleo Nchi yetu,Kwa Same serikali ya
Magufuli nakwenda kujenga Barabara kwa kiwango cha Rami kuelekea
Nkomanzi na Same Mashariki.
Wananchi wa
Mwigulu Nchemba akimndai Mathayo David Mgombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Vunjo kupitia CCM Ndg.Innocent Shirima hii leo.
Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi wa Vunjo kuwa Mabadiliko sio
vyama,Mabadiliko ni shughuli za maendeleo na Utendaji kazi.Magufuli
anakwenda kubadilisha Utendaji kazi na Usimamizi wake.
Picha na Sanga R.

Post a Comment