Vijana wengi wa kiume hujikuta katika wakati mgumu kuchukua maamuzi ya
kuishi na mwanamke japo yawezekana wakawa wanatamani kufanya hivyo kwa
muda mrefu kutokana na vikinza vingi, vingine vikiwa ni vya kimaisha na
vingine ni nadharia tu.
Katika bandiko hili, nitagusia sababu kadhaa zinazochangia vijana wengi kujikuta wakisuasua au kuogopa kuingia kwenye ndoa.
Kupanda kwa gharama za maisha
Kigezo hiki huwakumba zaidi wanaume ambao wanaishi mijini. Gharama za
maisha zimepanda sana kiasi kwamba mtu anaweza kuwa anaishi peke yake na
bado kuna mambo ambayo anashindwa kuyatimiza kwa wakati, kama vile kozi
ya nyumba, pesa ya kujikimu na mengine mengi. Wengi huona ni heri kuwa
na mtu tu ambaye ni mpenzi wake kuliko kudhibiti kabisa kwa kuwa na huyo
mtu kwa kuishi naye kwa hofu ya kushindwa kutimiza wajibu. Ndio maana
kwa wale ambao hupata akina dada ambao wanajiweza kujitegemea na hivyo
ni hodari kwa kusaidiana katika mambo ya kila siku hasa katika masuala
ya maendeleo huwa wepesi kuchukua maamuzi ya kuoa.
Utitiri wa wanawake wanaopatikana kirahisi bila hata kuoa
Ni suala ambalo lipo wazi hasa maeneo ya mijini akina dada/mama wa kuwa
nao katika mahusiano (bila kujalisha ni wa muda mfupi ama mrefu)
wamekuwa wengi, rahisi kuwapata, wa kila aina mwanaume watakao. Kuna
wanaume wamejikita katika hilo kiasi kwamba mradi tu atake mwanamke
atatoka/atatumia namba alizohifadhi kwenye simu na atafanikisha hiyo
azima yake ndani ya siku hiyo hiyo ambayo amedhamiria bila shida yoyote.
Hii inafanya kwa kiasi kuchangia kwa wanaume kusuasua katika maamuzi ya
kuoa. Kwa kimombo hujiambia, “If I can get it for free, why buy it?”
Maradhi hasa ugonjwa wa UKIMWI
Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDs kuwa
mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na
kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni
waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na
mtoto. Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko
kuingia katika ndoa. Naomba izingatiwe kuwa si wote; wengine huwa hodari
na huoa/olewa saa nyingine bila hata kumjulisha mpenzi wake huyo kuwa
yeye ana virusi chanya vya UKIMWI (HIV +ve).
Kufurahia ‘uhuru’
Hawa ni makapera wazoefu (wengine husema ‘bachela sugu’), hakuna mtu
ambaye anaweza mshawishi akabadilisha maisha yake hayo ya kikapela
(bachelor). Miaka huzidi kukatika hadi anafika miaka takribani 40 au
zaidi wala hana mpango wa kuoa na wala hajutii maamuzi yake hayo. Mara
nyingi wanaume wa namna hii hupenda sana wanawake (siyo lazima kuwa
atawachanganya kwa kuwa na zaidi ya mmoja); huwa na uwezo (hata kama
sustainable); Hutaka wanawake wadogo (mtu mzima sana kwake hapana hata
kama yeye ni mtu mzima); Ni mtu wa starehe sana, haoi kamwe na hufurahia
uhuru huo kwa hisia kuwa akioa ataupoteza uhuru wake.
Uhaba wa wanawake wanaofaa kuolewa
Na hii hutokea hasa kwa maeneo ya mijini. Wadada/mama wengi wamekuwa ni
‘wa mjini’ mno, wajanja, malengo mbele ikiwa imeambatana na tamaa,
wanaoweka pesa mbele utu nyuma, wachanganyi (kuwa na bwana zaidi ya
mmoja). Haya mambo yamekuwa yakifanywa bila kificho, inamfanya mwanaume
anapokuwa katika mahusiano ahisi kuwa hata mtu wake ana tabia hizo hizo
hata kama siyo kweli. Hii inakatisha tamaa kwa wanaume wengi na kuona
wanawake wanaofaa kuoa (tokana na viwango vyake alivyoweka) ni adimu ama
hawapo kabisa!
Kutopata ampendaye kwa dhati
Kuna wanaume vigezo vya mwanamke awe vipi havina umuhimu kabisa katika
kutaka kuamua kuoa. Yeye kikubwa anataka ampate mwamake ambaye atampenda
kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo mwanamke atampenda na
yeye pia kwa dhati. Huyu mwanaume anaamini msingi bora wa ndoa ni
mapenzi ya dhati kati ya yeye na mkewe basi! Hana haraka hadi pale
atakapompata mwanamke akampenda. Kama huyo mwanamke atakubali kuolewa
ama lah; hilo ni suala jingine!
Mahusiano mabovu ya awali
Kuna wanaume huchagua wanawake kwa sifa ambazo anazijua yeye mwenyewe.
Yeye hamuangalii mwanamke kama mtu, bali anamuangalia kama kitu. Daima
vigezo vyake ni nataka mwanamke wa hivi, tabia za vile, muonekano wa
kule na mambo mengine kedekede. Hivyo unakuta kila siku yuko katika
mahusiano na mwanamke ambaye ni kweli anampenda kimuonekano; ila
linapokuja suala la tabia wanashindwana kabisa. Anaachana nae kisha
anatafuta mwingine kwa mtindo uleule – mwisho wa siku analaumu wanawake
wote ni sawa na kukata tamaa ya kuoa ama kusuasua katika maamuzi ya
kutaka kuoa.
Kutoridhika na kipato chake
Kuna mwingine anaweza kuona kutoridhika na kipato (ni sawa na sababu ya
kwanza niliweka ya “Kupanda kwa gharama za Maisha”) – lakini hii ni
tofauti kidogo. Hapa namaanisha pale ambapo mwanaume ana uwezo kabisa wa
kuwa na mke na pia kuweza kukimu mahitaji yote pamoja na ya familia
yake. ILA kwa mipangilio yake anaona yeye bado; mara nyingi wa hivi
anataka ahakikishe ana uwezo wa kutosha ili aweze kuishi maisha ya
kifahari na si ya kujitosheleza tu. Hivyo katika hali ya kawaida ana
uwezo wa kuwa na mke lakini kwa maisha ya mtu wa kawaida na si wa
kitajiri kama malengo yake.
Malezi na Makuzi
Dhana mbovu juu ya ndoa
Dhana ya ndoa inaenda ikibadilika… Kumekuwa na tabia ya watu kukatisha
tamaa kwa kutoa vigezo, sababu, hadithi juu ya ndoa ambazo ni za kubomoa
kuliko kujenga. Sijui hawa watu hutumia vigezo gani… HATA siku moja
usitarajie uishi na mtu miaka nenda miaka rudi kitanda kimoja, nyumba
moja msigombane, kusiwe na madhaifu na pia kusiwe na wakati ambao wote
hadi kiwango cha kukata tamaa. Ndoa ni zaidi ya starehe na kufurahi…
Inahitaji nguvu kubwa, nguvu ya ziada, hekima, busara, kujituma na pia
kuwa committed kwa ndoa kuweza kufanikiwa. Sisemi kuwa lazima zote
zitafanikiwa maana kuna mambo ambayo yana mpaka – kuna wakati you just
let go. Ila hakuna haja ya kuibomoa hiyo taasisi kwa makusudi, taasisi
ambayo ni msingi bora wa malezi ya watoto kuliko taasisi yoyote ile
inayoweza lea watoto ambao hasa ndiyo tegemeo la vizazi vijavyo.
Kuzaa ovyo/Kuzaa kabla ya ndoa
Kuna wanaume wanazalisha balaa! Bila kujalisha hizo mimba ni zao kweli
ama wamesingiziwa kinachojalisha na watoto hao kawakubali na anawalea.
Kuna wanaume hadi anafikia umri wa miaka 30 tayari ana watoto wa
wanawake tofauti hata watano na analea. Kwa kiasi fulani, hii inaweza
mvunja morali ya kutaka kuoa, anaona kama watoto tayari anao na anawalea
hivyo hakuna haja ya kuwa na mwanamke kabisa ndani kama mke. Hii ni
mara chache.
Kukua kwa idadi ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa
Maadili mengi ya wanandoa yamezidi kushuka… Hapo nyuma ilishazoeleka
wanaume huwa na tabia ya kutoka nje ya ndoa na wanawake kwa uchache.
Bahati mbaya siku zinavyozidi kwenda idadi ya wanawake wanaotoka nayo
inakuwa kwa kasi, tabia ambayo inafanywa bila kificho kabisa na imekuwa
kana kwamba ni mashindano ya kutoka. Ni wazi thamani (reputation) ya
mwanamke ambaye anatoka na mwanaume anayetoka ni tofauti. Ni wanaume
wachache wana kifua cha kuweza kuvumilia mkewe/mpenziwe kutoka nje na
kuendelea kuwa naye. Kwa wanaume wengi ambao hawajaoa hili huchangia
katika kukata tamaa ya kupata mwanamke ambae anafaa kuwa mke na
asiyeweza kuwa msaliti.
TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
During its two year run, the project will award approximately 100 major
reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for
stories on development issues.
Journalists who produce the best stories published or broadcasted in
media that reach African audiences, will win a major international
reporting trip.
During its two year run, the project will award approximately 100 major
reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for
stories on development issues. Journalists who produce the best stories
published or broadcasted in media that reach African audiences, will win
a major international reporting trip.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;
Filed Under:
UDAKU
on Monday, 28 September 2015
Post a Comment