Featured

Loading...


TASWIRA ZA JK AKIWA UMOJA WA MATAIFA, NEW YORK, KWA MARA YA MWISHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana jumanne amelihutubia kwa mara ya mwisho Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mtaifa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hotuba ya Mhe. Rais na ambayo iligusia mambo mengi ya kisiasa, kiuchumi, na maendeleo akitumia pia fursa hiyo kuwaanga viongozi wenzie na kuwashukuru kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake, iliwasisimua wajumbe wa mkutano huo kiasi cha kukatishwa mara kwa mara kwa makofi.


Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazomwonyesha Mhe. Rais katika Matukio mbalimbali Moja wapo likiwa ni hafla ambayo Rais wa Marekani, Mhe Barack Obama aliiandaa kwaajili wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Picha kwa hisani ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Barack Obama na Mkewe Michelle Obama wakati wa hafla ilioandaliwa na Rais wa Marekani kwaajii ya Viongozi wa Wakuu Nchi na Serikali wanaohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ( Picha hii ni kwa hisani ya Ofisi ya Itifaki ya White House)


Mhe. Rais Kikwete akiwa na Mhe. Sophia Simba, Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula na mwanamitindo Flaviana Matata muda mfupi mara baada ya kulihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa


Mwakilishi wa Kudumu wa Antigua na Bermuda Balozi Walton Alfonso Webson ambaye ni mlemavu wa kutoona akimwongoza Mhe. Rais Kikwete kwenda kuonana na Waziri Mkuu wake, Mhe. Gaston Alphoso Browne aliyekuwa na mazungumzo wa Mhe.Rais mara baada ya Mhe. Rais kulihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa.


Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Mhe. Gaston Alphonso Browne, wengine katika mazungumzo hayo ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa kudumu wa Antigua na Barbuda, Balozi Walton Webson mwenye miwani myeusi na Mkurungezi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestin Mushy

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top