Featured

Loading...


Bawacha: Wanawake Mkipiga Kura Kaeni Mita 200 Mzilinde Zisiibiwe

BARAZA la Wanawake la Chama Cha Demokrasia (Chadema) Taifa, Bawacha, limewataka wanawake nchi nzima kupiga kura na kukaa mita 200 ili kulinda kura zao kwani ni haki yao kisheria.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha Kunti Yusuph wakati wa mkutano na wanawake, uliofanyika katika ofisi za Chadema kanda ya ziwa Victoria jijini Mwqanza.

Mkutano huo uliohudhuliwa na wanawake wengi na kusababisha watu walio wengi kukosa eneo la kukaa kutokana na kunyimwa Uwanja wa Baptist uliopo kona ya Bwiru na halmashauri ya manispaa ya Ilemela, dakika za mwisho licha ya kuwepo taarifa.

Kunti alisema kwa mujibu ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010, inamruhusu mtu kupiga kura na kukaa mita 200, kutoka kwenye kituo lakini serikali ya CCM inawakataza wananchi kwa kisingizio cha usalama kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

“Katika Taifa lolote lile haijawahi kutokea kwamba ukipiga kura uende nyumbani, ndiyo mara ya kwanza kuona kwa Tanzania, hatuwezi kuondoka tutabaki mita 200,” alisema Yusuph.

Kunti ambaye ni mratibu wa mikutano ya kukutana na wanawake ya mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa, alisema kuwa kupitia wanawake wa Mwanza, wanawake nchi nzima wanapaswa kupiga kura na kulinda kura zao.

Alisema endapo wanawake na watanzania kwa ujumla watapiga kura na kuondoka watakuwa wamevunja sheria ya nchi hivyo amewaomba kulinda kura zao kwani ndio maisha yao.

Kwa upande wake Mama Regina Lowassa, alikivaa Chama cha Mapinduzi (CCM) kushindwa kuongea ni nini watawafanyia watanzania na badala yake wamegeuka watukanaji jukwaani.

“Kama CCM wana nia njema na watanzania, kwa nini wasimame jukwaani na kuanza kutukana ninawaomba Wanawake msitishike na watu wa aina hiyo,” alisema Mama Regina.

Pia alisema kuna watu wachache ambao wamekusudia kuharibu uchaguzi kwa lengo la manufaa yao binafsi kitendo ambacho watanzania wanapaswa kuacha kukata tamaa.

Hata hivyo Regina aliwaomba wanawake na watanzania kwa ujumla kukichagua Chadema kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na nafasi ya Urais kwa maendeleo ya Taifa.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top