Featured

Loading...


Helkopta Nyingine ya Mgombea Ubunge CCM Yapata Hitilafu..Mgombea Ashtukia Aaapa Kuto Ipanda Tena.....

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde ameapa kutotumia tena usafiri wa anga katika kampeni, baada ya helikopta aliyokuwa anatumia kupata hitilafu na kushindwa kuruka katika Kijiji cha Idifu wilayani hapa, juziLusinde maarufu kwa jina la Kibajaji alithibitisha kuwa helikopta hiyo ilishindwa kuruka baada ya rubani kubaini ilikuwa na hitilafu, na ilikuwa imetua katika eneo la kichaka kijijini hapo.
Jana asubuhi alifika mtaalamu wa ndege kutoka Afrika Kusini na kuirusha hadi Dodoma Mjini.
“Ni kweli kuna tatizo hilo na hadi sasa (juzi) tunasubiri mafundi kutoka Dar es Salaam ili waje kuikagua na kujua tatizo lake nini,” alisema Lusinde, ikiwa ni siku moja baada ya helikopta nyingine kuanguka na kuua abiria wanne akiwamo mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe.
Kutokana na hali hiyo, Lusinde alisema, “Hata wakinipa ndege nyingine siwezi kuitumia tena, nimeamua kuwa ardhini na kama kufa bora nifie chini lakini siyo angani. Nasema katika kampeni hizi situmii anga tena na sababu kubwa ni kuwa zaidi ya wananchi wangu 500 wamepiga simu kunisihi nisitumie usafiri wa anga kipindi hiki”. Mgombea huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na mmoja wa wajumbe wa timu ya kampeni za mgombea urais wa chama hicho, alisema wakati ndege hiyo ikishindwa kuruka alikuwa amefanya mikutano mitatu jimboni kwake na alitarajia kumaliza kisha kuendelea katika mikoa aliyopangiwa kumnadi Dk John Magufuli.

Aliwataja waliokuwamo kwenye helikopta hiyo kuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Chamwino, Devotha Mbogoni; Katibu Mwenezi wa CCM wilaya, Marietha Mkuya; Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Mvumi Mission, Mathias Lusano na yeye na kwamba, wote walitoka wakiwa
CHANZO MWANANCHI

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top